Muigizaji wa filamu adai kunyanyaswa kijinsia na George Bush


Picha ya bwana Barrack Obama akimsalia rais huyo wa zamani ilimkasirisha msichana huyo.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPicha ya bwana Barrack Obama akimsalia rais huyo wa zamani ilimkasirisha msichana huyo.
Aliyekuwa rais wa Marekani George Bush ameomba msamaha kwa dhiki aliyosababisha baada ya muigizaji mmoja kumtuhumu wa kumnyanyasa kijinsia.
Heather Lind alisema kuwa rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 93 alimshika kutoka nyuma akiwa katika kiti chake cha magurudumo na kutamka ''mzaha mchafu'' wakati wakijiandaa kupiga picha.
Bi Lind alitoa madai hayo katika mtandao wa Instagram katika chapisho ambalo limefutwa.
Msemaji wa Bush alisema kuwa kisa hicho kilikuwa jaribio la ucheshi.
''Rais Bush alikuwa hawezi chini ya hali yoyote ile na kwa makusudi kumsababishia mtu dhiki na ameomba msamaha iwapo kitendo chake cha kuzua ucheshi kilimkosea bi Lind'', taarifa iliosambazwa kwa vyombo vya habari ilisema.
Bi Lind anasema kuwa kisa hicho kilitokea 2014Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBi Lind anasema kuwa kisa hicho kilitokea 2014
Mitandao yote ilihifadhi chapisho hilo la Lind kabla ya kufutwa.
Bwana Bush alihudumu katika kipindi cha miaka mitano kutoka 1989 hadi 1993 na ni babake George W Bush ambaye alihudumu mihula miwili kati ya 2001 hadi 2009.
Mzee huyo anaugua ugonjwa wa kutetemeka.
Muigizaji wa filamu adai kunyanyaswa kijinsia na George Bush Muigizaji wa filamu adai kunyanyaswa kijinsia na George Bush Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 26, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...