Uchaguzi Kenya: Mkuu wa tume ya uchaguzi Wafula Chebukati akutana na Raila Odinga

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Kenya Wafula Chebukati akutana na mgombea urais wa upinzani Raila Odinga.
Bw Chebukati amesema anatarajia kukutana na mgombea wa chama tawala cha Jubilee Uhuru Kenyatta baadaye.
"Mkutano huo utafuatwa na mkutano wa pamoja wa wawili hao," ameandika kwenye Twitter.
Gazeti la kibinafsi la Nation limesema wawili hao walikutana kwa takriban dakika 40 katika makao makuu ya tume hiyo Nairobi.
Mwenyekiti huyo alikuwa awali ameitisha mkutano wa wagombea urais wote leo adhuhuri lakini akauahirisha mapema leo asubuhi.
Uchaguzi mpya umepangiwa kufanyika Alhamisi wiki ijayo.
Hata hivyo, ingawa Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza yuko tayari kwa uchaguzi huo na utaendelea, mgombea wa upinzani Raila Odinga alijiondoa wiki iliyopita.
Jana, Bw Odinga, ambaye ni mgombea wa muungano wa National Super Alliance (Nasa) alitangaza kwamba siku hiyo badala ya kushiriki uchaguzi, wafuasi wake watafanya maandamano makubwa kote nchini.
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati siku ya Jumatano alikuwa amewalaumu wanasiasa wa kusababisha kuwepo kwa mazingira yanayoifanya vigumu kuandaa uchaguzi huru na wa haki.
Alisema alikuwa anawapa "kadi ya manjano".
Waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang'i tayari ametangaza Alhamisi kuwa siku ya mapumziko.
Uchaguzi Kenya: Mkuu wa tume ya uchaguzi Wafula Chebukati akutana na Raila Odinga Uchaguzi Kenya: Mkuu wa tume ya uchaguzi Wafula Chebukati akutana na Raila Odinga Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 19, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...