Umoja wa Mataifa wataka wapinzani 30 kuachiwa huru DRC


Wapinzani wakiandamana nchini DR Congo
Image captionWapinzani wakiandamana nchini DR Congo
Umoja wa mataifa umetoa wito ya kuachiwa mara moja kwa watu 30, wa chama kikuu cha upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kutoka korokoroni.
Wanachama wa vyama vikuu viwili vya Union for Democracy na wenzao wa Social Progress, walikamatwa siku ya Jumapili katika mji wa Lubumbashi, ulioko Kusini mashariki mwa nchi hiyo, baada ya polisi kuvunja mkutano waliokuwa nao.
Utawala wa Rais, Joseph Kabila, umepiga marufuku mkutano wa aina yoyote wa kisiasa, pamoja na maandamano ya upinzani, tangu muda wake wa kuhudumu kama Rais kisheri, ulipomalizika mwaka mmoja uliopita.
Rais Joseph Kabila amesalia mamlakani hata baada ya muhula wake kuhudumu kumalizika mwaka mmoja uliopitaHaki miliki ya pichaBBC SPORT
Image captionRais Joseph Kabila amesalia mamlakani hata baada ya muhula wake kuhudumu kumalizika mwaka mmoja uliopita
Tume ya uchaguzi nchini humo, imesema kuwa, haitakuwa rahisi kuandaa uchaguzi mkuu wa Urais, kabla ya mwezi Aprili mwaka ujao wa 2019.
Chama kingine cha upinzani- Union for the Congolese Nation, kimesema kwamba, kitajiondoa katika serikali ya ugawanaji mamlaka, kuhusiana na kucheleweshwa kwa uchaguzi mkuu.
Maandamano ya mara kwa mara ya upinzani nchini humo umekabiliwa vikali na utawala wa Rais Joseph Kabila.
Umoja wa Mataifa wataka wapinzani 30 kuachiwa huru DRC Umoja wa Mataifa wataka wapinzani 30 kuachiwa huru DRC Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 24, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...