KIPA CLAUDIO BRAVO APANGUA PENATI NA KUIPELEKA MAN CITY ROBO FAINALI


Kipa Claudio Bravo ameibuka kuwa shujaa wa Manchester City katika mchezo wa jana dhidi ya Wolves baada ya kupangua mikwaju ya penati na kutinga robo fainali ya kombe la Carabao.

Bravo, aliyeokoa michomo mitatu katika muda wa kawaida aliongeza kuonyesha ushujaa wake kwa kupangua penati za Alfred N'Diaye na Conor Coady baada ya mchezo kuisha kwa sare tasa.

Manchester City ilifunga penati zote nne huku, Sergio Aguero kumalizia kiufundi penati ya nne na kufanya matokeo kuwa 4-1.
         Kipa wa Manchester City Claudio Bravo akipangua penati ya Alfred N'Diaye
                       Sergio Aguero akishangilia baada ya kutumbukiza golini mpira wa penati
KIPA CLAUDIO BRAVO APANGUA PENATI NA KUIPELEKA MAN CITY ROBO FAINALI KIPA CLAUDIO BRAVO APANGUA PENATI NA KUIPELEKA MAN CITY ROBO FAINALI Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 25, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...