Manchester United yailaza Benfica ugenini

Kipa Mile Svilar alidondokwa na machozi baada ya kufungwa bao hilo na ikamlazimu M'belgiji mwenzake Lukaku kumnyamazisha

Haki miliki ya pichaREX FEATURES
Image captionKipa Mile Svilar alidondokwa na machozi baada ya kufungwa bao hilo na ikamlazimu M'belgiji mwenzake Lukaku kumnyamazisha
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa sio uhalifu ''kuweka basi'' nyuma huku kikosi chake kikiishinda Benfica katika mechi ya vilabu bingwa Ulaya.
Bao la pekee mjini Lisbon lilifungwa na Marcus Rashford aliyepiga mkwaju wa adhabu na kumwacha kipa wa Benfica Mile Svilar bila jibu.
Svila ambye ni raia wa Ubelgiji na kipa mwenye umri mdogo zaidi aliupangua mpira huo katika goli lake.
Hatahivyo Rashford alikitia wasiwasi kikosi cha United baada ya kutoka nje akiguchia katika kipindi cha pili na mahala pake pakachukuliwa na Anthony Martial.
United walikosolewa kwa mchezo wao katika sare ya 0-0 dhidi ya Liverpool siku ya Jumamosi ambapo walifanya shambulio moja pekee , lakini sasa The Red Devils wamefungwa mabao sita msimuu huu.


Manchester United yailaza Benfica ugenini Manchester United yailaza Benfica ugenini Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 19, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...