Leicester City 1-1 West Bromwich

Awali Mahrez alipoteza nafasi nyingi za magoli

Image captionAwali Mahrez alipoteza nafasi nyingi za magoli
Goli la kwanza kwa Riyad Mahrez msimu huu liliinusuru Leicester City kuondoka bila alama nyumbani kwake ilipovaana na West Bromwich.
Nacer Chadli aliiandikia West Bromwich goli la kuongoza dakika ya 63.
Mahrez alipoteza nafasi nyingi za wazi kabla ya Islam Slimani aliyeingia dakika ya 74 kumtengenezea pande safi na kuiandikia Leicester mabingwa wa 2015-16 goli dakika ya 80.
Ni mara ya tatu msimu huu West Brom inakubali goli la kusawazisha baada ya dakika 75.
Wachezaji wakipongezana baada ya mchezo
Image captionWachezaji wakipongezana baada ya mchezo
Leicester inasalia kwenye timu tatu za mwisho ikiwa haijashinda michezo sita ya ligi kuu.
Mara ya mwisho kucheza michezo sita bila kushinda, Claudio Ranieri alifukuzwa nafasi ya ukocha.
Leicester City 1-1 West Bromwich Leicester City 1-1 West Bromwich Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 16, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...