Mwandishi maarufu auawa visiwa vya Malta

Malta

Haki miliki ya pichaLINKEDIN
Image captionDaphne Caruana Galizia mwandishi nguli wa habari za uchunguzi aliyeuawa katika mlipuko wa bomu
Mwandishi nguli wa habari za uchunguzi katika visiwa vya Malta ameuawa wakati gari alilokuwa akiliendesha lilipolipuliwa na bomu kubwa upande wa Kaskazini ya kisiwa hicho.
Daphne Caruana Galizia amekuwa akiitumia blogu yake kuandika taarifa zihusianazo na kesi za madai ya rushwa , zikiwemo za wanasiasa nguli visiwani humo.
MaltaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captioneneo la tukio Malta
Wakati wa uhai wake likuwa akimshutumu waziri mkuu wa visiwa hivyo, Joseph Muscat, na mkewe kutumia akaunti za benki za siri ili kuficha malipo kutoka kwa familia ya utawala wa Azerbaijan suala ambalo waziri mkuu na familia yake wamelikana.
Bwana Muscat ameyaita mauaji hayo kama kuua tendo baya kuwahi kutokea visiwani na kuahidi kuwa atahakikisha waliotekeleza tukio hilo na muuaji wanafikishwa katika mkono wa sheria.
Mwandishi maarufu auawa visiwa vya Malta Mwandishi maarufu auawa visiwa vya Malta Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 16, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...