JULIO ALIA NA TFF, ANATAKA DODOMA FC IPANDISHWE DARAJA

Timu ya Mwadu FC ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Toto Africans kwenye mchezo wake wa mwisho wa Ligi Daraja la Kwanza lakini ushindi huo haukuiwezesha Dodoma FC kupanda daraja.
Hiyo ilitokana na kuwa tayari, Alliance Schools ya Mwanza na Biashara ya Musoma  ndizo zilizopata nafasi katika Kundi Kundi C ambapo sasa zitacheza Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao.
Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihweo ‘Julio’ amesema kuwa wamekubali matokeo ya uwanjani lakini akasema lawama zake anazipeleka Bodi ya Ligi kwa kuwa huko kuna rufaa yao wanayosubiri majibu.
Julio amesema walipeleka malalamiko juu ya wapinzani wao kumtumia mchezaji ambaye hakuwa na leseni, lakini kilichotokea uwanjani hakuwa na lolote la kubadilisha.
Pamoja na hivyo, Julio amesema ikitokea rufaa yao haijafanyiwa kazi au ikapigwa chini bado wanao nafasi ya kufanya kweli msimu ujao.
“Tunaamini malalamiko yetu ni halali na yana msingi imara kwa hiyo tutakata rufaa kupitia TFF chombo cha juu ambacho tunafikiri watatenda haki. Mimi bado naamini tuna nafasi ya kucheza ligi kuu,” alisema Julio.
JULIO ALIA NA TFF, ANATAKA DODOMA FC IPANDISHWE DARAJA JULIO ALIA NA TFF, ANATAKA DODOMA FC IPANDISHWE DARAJA Reviewed by RICH VOICE on Februari 05, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...