Makamu rais wa Marekani agoma kula chakula cha jioni na dada rais wa Korea Kaskazini

pence

Makamu rais wa Marekani, Mike Pence amegoma kuwepo katika chakula cha jioni ambacho alitakiwa kukaa meza moja na kiongozi wa serikali ya Korea Kaskazini Kim Yong-nam.
Taarifa kutoka chombo cha habari cha Yo hap kimesema kuwa Pence alionana kidogo na bwana Kim wakati wakijaribu kukwepana kuonana uso kwa uso.
Wakati huo huo, rais wa Korea ya Kusini Moon Jae-in ameshikana mikono na dada yake kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong un katika sherehe za ufumbuzi wa mashindano ya michezo ya Olympiki ya msimu wa baridi.
Michezo hiyo inaendelea wakati ambapo kuna mvutano juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.
Pence alimleta Fred Warmbier kama mgeni Korea Kusini, baba wa kijana mdogo wa Marekani aliyekufa baada ya kutolewa gerezani huko Korea Kaskazini.
Bwana Pence na Kim Yong-nam walikuwa wenyeji wa rais wa Korea Kusini kabla ya sherehe haijaanza huko Pyeongchang.
korea
Lakini Makamu rais wa Marekani alikaa kwenye tafrija hiyo kwa dakika tano tu na kuondoka.
Katika shughuli hiyo, Bwana Moon alisema anatarajia mashindano hayo ya michezo ya Olimpiki msimu wa baridi yataweza kukumbukwa kama siku nzuri ya kuanza kuwa na amani.
Hata hivyo ziara yake inaonekana kuwa ishara kwamba Kim Jong un yuko tayari kuimarisha uhusiano na Korea Kusini ,nchi ambazo zilikuwa katika mvutano kwa kipindi kirefu.
Makamu rais wa Marekani agoma kula chakula cha jioni na dada rais wa Korea Kaskazini Makamu rais wa Marekani agoma kula chakula cha jioni na dada rais wa Korea Kaskazini Reviewed by RICH VOICE on Februari 09, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...