Upinzani kupinga matokeo ya uchaguzi Guinea

media 
Viongozi wa upinzani nchini Guinea mwishoni wametupilia mbali uchaguzi wa serikali za mitaa na kusema kuwa ni ulaghai ulio wazi uliofanyika kwenye nchi hiyo ya Afrika magharibi, na kwamba uchaguzi huo ulicheleweshwa katika sehemu mbali mbali serikali ikilenga kufanya udangayifu.
Watu milioni sita walitakiwa kupiga katika uchaguzi huo wa kwanza, tangu mwaka 2005.
Upinzani unadai kuwa uchaguzi wa Jumapili uligubikwa na udanganyifu mkubwa, utumiaji vibaya wa kura, na kuna watu walipiga kura zaidi ya mara moja.
Lakini Jacques Gbonimy, mmoja kati ya maafisa wa Tume ya Uchaguzi (Ceni), amejaribu kujitetea akisema: "Katika baadhi ya majimbo, baadhi walisema kuwa muda wa kupiga kura uliongezwa hadi 20h. Ceni haikutoa uamuzi huo. Uchaguzi ulikwenda vizuri.


 Aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Sidya Toure amewaambia wanahabari kuwa wapinzani wana uthibitisho kuwa Kuna udanganyifu mkuwa ambao ulifanyika katika ngazi ya kitaifa, ambao ulianzia katika vituo vya kupigia kura, hivo hawatakubali matokeo yoyote ya uchaguzi huo.
"Tuna wakuu wa wilaya na wasaidizi wao, walianaweza kuchukua vifaa vyote vya uchaguzi na kuomba kwamba zoezi hilo likafanyikie nyumbani kwao au ofisini kwao. Na waliweza kuzuia kuingia kwa wawakilishi wa vyama vingine, hasa wale wa upinzani. "
 
Waziri mkuu wa zamani na kiongozi wa chama cha UFR, Sidya Toure. AFP PHOTO / CELLOU BINANI
Waziri mkuu wa zamani na mkuu wa chama kikuu cha upinzani cha UFDG, Cellou Dalein Diallo, amesisitiza akisema: "Nimetoa wito kwa wananchi wanaotaka demokrasia kusonga mbele kupinga mchakato hu wa uchaguzi ambayo Bw Alpha Condé na familia yake wanajiandaa kwa uchaguzi huu wa mitaa.
Makabiliano yalizuka kati ya wapiga kura wa vyama hasimu au wafuasi wa upinzani na polisi nchini kote ikiwa ni pamoja na mji mkuu wakati wa kuhesabu kura au wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi.
Upinzani kupinga matokeo ya uchaguzi Guinea Upinzani kupinga matokeo ya uchaguzi Guinea Reviewed by RICH VOICE on Februari 05, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...