Tanzania kuwa na watu 58 milioni ifikapo mwishoni mwa mwaka huu

Tanzania inatarajiwa kufikisha idadi ya watu milioni 58 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la juu ikilinganishwa na idadi ya awali ya watu milioni 46 iliyoripotiwa mwaka 2010.

Kwa mujibu wa Idara ya Jamii na Mambo ya Uchumi ya Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), makadirio hayo ni sawa na kila kilomita moja ya mraba kuna wakazi 67 tofauti na makadirio ya mwaka 2010 ya watu 52.

“Tanzania ina kiwango kikubwa cha kuzaliana duniani na zaidi ya asilimia 44 ya watu ni chini ya miaka 15. Kiwango cha kuzaliana ni watoto 5.01 kwa mwanamke mmoja ambacho ni kikubwa kwa nchi kama Tanzania,” ripoti hiyo ya makadirio ya UN inaonyesha.

Inasema kila sekunde 14, mtoto mmoja anazaliwa nchini huku mtoto mmoja akifariki dunia kila baada ya sekunde moja.

Makadirio hayo pia yanaonyesha kuwa idadi ya watu nchini imeongezeka kwa asilimia 3.15 kwa kipindi cha miaka minane iliyopita wakati kiwango cha kuzaliana kilikuwa ni asilimia 5.17 kati ya mwaka 2015 na 2018.

Ikiwa hali hiyo itaendelea hivyo, ripoti hiyo inabainisha kuwa kwamba idadi ya watu itaongezeka kufikia milioni 95.5 ifikapo mwaka 2050 na watu milioni 300 ifikapo mwaka 2099.

Mchanganuo wa ripoti hiyo unaonyesha kuwa makadirio hayo ni sawa na asilimia 0.77 ya idadi ya watu duniani kwa mwaka huu kutoka asilimia 0.66 katika mwaka 2010.

Tanzania imewekwa katika nafasi ya 24 miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya watu duniani mwaka huu, kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na mwaka 2010 ambapo ilikuwa nafasi ya 28.

Idadi ya hivi sasa ya watu waishio mijini inakadiriwa kufikia milioni 19.2 sawa na asilimia 31 ya idadi ya watu wote ikilinganishwa na ile ya awali ya mwaka 2010 iliyokuwa milioni 12.6 ambayo ilikuwa sawa na asilimia 27.4.

Hata hivyo, kulingana na makadirio ya idadi ya watu nchini mwaka 2016-17 yaliyofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ilikadiriwa kwamba kungekuwa na idadi ya watu milioni 51.55 katika kipindi cha mwaka jana.
Tanzania kuwa na watu 58 milioni ifikapo mwishoni mwa mwaka huu Tanzania kuwa na watu 58 milioni ifikapo mwishoni mwa mwaka huu Reviewed by RICH VOICE on Februari 08, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...