WATFORD YAICHAKAZA CHELSEA NA KUWEKA KIBARUA CHA CONTE REHANI

Watford imefunga magoli matatu ya dakika za mwisho na kumpatia ushindi wa kwanza nyumbani kocha Javi Gracia katika usiku ambao hautosahaulika na kocha huyo mpya baada ya kuichakaza Chelsea magoli 4-1.

Timu ya Chelsea inayonolewa na Antonio Conte ambaye anakabiliwa na shinikizo la kutimuliwa kibarua chake ilicheza saa zima wakiwa na wachezaji 10 baada ya Tiemoue Bakayoko kupewa kadi nyekundu.

Watford ilipata magoli yake kupitia kwa Troy Deeney kwa mkwaju wa penati baada ya Thibaut Courtois kufanya madhambi, lakini Eden Hazard akasawazisha dakika ya 82. 
Daryl Janmaat akafunga goli la pili dakika ya 84 na Gerard Deulofeu la tatu dakika ya 88 huku naye Roberto Pereyra akifunga goli la nne dakika ya 90+1. 
                                  Eden Hazard akiachia shuti na kufunga goli pekee la Chelsea
                            Roberto Pereyra akiachia shuti na kufunga goli la nne la Watford 
WATFORD YAICHAKAZA CHELSEA NA KUWEKA KIBARUA CHA CONTE REHANI WATFORD YAICHAKAZA CHELSEA NA KUWEKA KIBARUA CHA CONTE REHANI Reviewed by RICH VOICE on Februari 06, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...