PHILIPPE COUTINHO AANZA KUFUNGUA AKAUNTI YA MAGOLI BARCELONA

Philippe Coutinho amefunga goli lake la kwanza akiwa na Barcelona na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Valencia na kutinga fainali ya Copa del Rey.

Coutinho, akicheza kwa mara ya tano tangu uhamisho wa paundi milioni 142 akitoka Liverpool aliingia katika kipindi cha pili na kufunga goli kufuatia krosi ya Luis Suarez.

Barcelona ambao ni mabingwa mara tatu mfululizo wa Copa del Rey ilipata goli lake la pili kupitia kwa Ivan Rakitic.
                       Lionel Messi akimpongeza Philippe Coutinho baada ya kufunga goli
                          Luis Suarez akipambana na kipa Jeume Domenech wa Valencia
PHILIPPE COUTINHO AANZA KUFUNGUA AKAUNTI YA MAGOLI BARCELONA PHILIPPE COUTINHO AANZA KUFUNGUA AKAUNTI YA MAGOLI BARCELONA Reviewed by RICH VOICE on Februari 09, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...