Kim Jong-un aishukuru Korea Kusini kwa makaribisho mema

Photo of the North Korean delegation and Mr KimKiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ameisifu Korea Kusini kwa jitihada zake nzuri za kuukaribisha ujumbe kutoka Kaskazini wakati wa mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi.
Matamshi yake yanakuja huku ujumbe, ulioongozwa na dada yake Kim Yo-jong uliporejea nyumbani kutoka Pyeongchang.
Shirika la habari la serikali KCNA lilisema kuwa Bw Kim aliishukuru Korea Kusini kwa kuupigia debe uwepo wake katika mbio hizo.
Kuhudhhuria kwa Korea Kaskazini kumekuwa kwa mchango mkubwa kwa uhusiani kati ya nchi hizo.
Lakini kumekuwa pia na wasi wasi kuwa hiyo imeruhusu Korea Kaskazini kufanikiwa katika propaganda zake.
Bi Kim na mkuu wa nchi asiye na madarakani Kim Yong-nam waliakuwa miongoni mwa maafisa wakuu waliokuwa kwenye ujumbe wa Korea Kaskazini kuzuru Korea Kusini tangu vita vya Korea Kaskazini miaka ya 1950.
Sikua ya Jumamosi Kim alimualika rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, kuzuru Pyongyang kwa mazungumzo. Ikiwa mkutano huo utafanyika utakuw wa kwanza kwa zaidi ya muongo mmoja kati ya viongozi wa Korea mbili.
Mwaliko huo unakuja hukua uhusino kati ya Korea zote ukionekana kuboreka.
Kim Jong-un aishukuru Korea Kusini kwa makaribisho mema Kim Jong-un aishukuru Korea Kusini kwa makaribisho mema Reviewed by RICH VOICE on Februari 13, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...