Muhubiri nchini Rwanda asema wanawake ''ni chanzo cha uovu'' duniani

Muhubiri mmoja nchini Rwanda amesema kuwa wanawake ''ni chanzo cha uovu'' wote duniani

Muhubiri mmoja wa Rwanda huenda akajapata mashakani mbele ya vyombo vya habari baada ya kuwaita wanawake ''chanzo cha uovu'' katika mahubiri ya redio.
Muhubiri hiyo wa kanisa la Seventh Day Adventist Nicolas Niyibikora aliwambia wanawake kwamba hawapendwi na Mungu wakati wa matangazo ya idhaa ya redio ya Amazing Grace mwezi Januari akionya kuwa ''hakuna lolote jema linaloweza kupatikana kutoka kwa wanawake''.
''Unaposoma Biblia , ni nani aliyeleta dhambi duniani''? Aliuliza akiongeze, ''sio mwanamume''.
Tayari mahubiri hayo yamewakasirisha wanaharakati huku wale wanaounga mkono usawa wa kijinsia wakiitisha mkutano na vyombo vya habari na kuonya kuwa maneneo kama hayo yanaweza kusababisha chuki na mzozo miongoni mwa raia wa Rwanda iwapo hakuna hatua ya haraka itachukuliwa , kulingana na gazeti la Rwanda la New Times.
Kundi la kutetea haki za wanawake liliwasilisha malalamishi yake katika tume ya udhibiti wa vyombo vya habari ambayo inatarajiwa kukutana ili kuzungunmzia kuhusu swala hilo wiki ijayo.
Afsa mkuu Emmanuel Mugisha aliambia gazeti la New Times kwamba kuna uwezekano idhaa hiyo italazimika kujieleza.
Kanisa la Seventh Day nchini Rwanda limefanya juhudi za kujitenga na Niyibikora, ambaye wanasema aliipgwa marufuku kwa miaka ,mitano.
Muhubiri nchini Rwanda asema wanawake ''ni chanzo cha uovu'' duniani Muhubiri nchini Rwanda asema wanawake ''ni chanzo cha uovu'' duniani Reviewed by RICH VOICE on Februari 09, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...