TOTTEHAM YAPAMBANA NA KULAZIMISHA SARE NA LIVERPOOL DAKIKA ZA NYONGEZA

Mkwaju wa penati wa Harry Kane umeiwezesha Tottenham kuambulia sare ya magoli 2-2 katika dakika za nyongeza baada ya goli la dakika 90 la Mohamed Salah kuonekana kama lingeipa ushindi Liverpool.

Liverpool ilikuwa imebakiza sekunde chache tu kuibuka na ushindi lakini refa Jon Moss alitoa penati baada ya beki Virgil van Dijk kumchezea rafu Erik Lamela, na Kane aliyekuwa amekosa penati ya kwanza kurekebisha makosa na kufikia goli la 100.

Katika mchezo huo Salah alifunga goli ndani ya dakika tatu, baada ya kuiwahi pasi mbaya ya kurudisha nyuma mpira ya Eric Dier na kuipatia Liverpool goli lililodumu hadi dakika ya 80 pale Victor Wanyama aliyetokea benchi kuachia shuti kali lililomshinda kipa Loris Karius.
        Mshambuliaji Raia wa Misri Mohamed Salah akifunga goli la pili la Liverpool 
Mshambuliaji Muingereza Harry Kane akifunga goli la kusawazisha kwa mkwaju wa penati na kufanya matokeo kuwa 2-2

TOTTEHAM YAPAMBANA NA KULAZIMISHA SARE NA LIVERPOOL DAKIKA ZA NYONGEZA TOTTEHAM YAPAMBANA NA KULAZIMISHA SARE NA LIVERPOOL DAKIKA ZA NYONGEZA Reviewed by RICH VOICE on Februari 05, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...