Amber Lulu: Simpendi Baba Yangu Hata KIdogo Na Wala Sitaki Kumuona
Video vixen maarufu aliyegeukia sanaa ya Bongo fleva Amber Lulu amekiri kuwa amemtosa Baba yake mzazi na hataki hata kumuona.
Amber
Lulu amefunguka hayo wakati anaelezea changamoto alizozipitia katika
maisha yake baada ya Baba yake mzazi kuwakimbia na kumuacha yeye kama
mtu pekee ambaye alitakiwa kuiangalia familia yake hasa mama yake ambaye
alikuwa mgonjwa.
Amber
Lulu ameongelea uhusiano aliokuwa nao na Baba yake mzazi ambapo amekiri
katika umri mdogo alianza kushika majukumu mazito ya kuielea familia
yake hivyo ilimbidi ajiingize katika biashara mbali mbali ili aweze
kupata pesa.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds Fm, Amber Lulu aliongea haya kuhusiana na changamoto alizozipitia:
"Kipindi
hiko nilikuwa bado niko shule lakini ilikuwa likizo hata ya wiki mbili
nilikuwa nakuja Dar kufanya kazi maana tulikuwa tunahitaji pesa na mama
Yangu alikuwa mgonjwa na ndio baba alikuwa kashatukimbia, nakumbuka
msanii alikuwa anaitwa Pasha alinitumia kwenye video yake akanilipa
shilingi elfu hamsini ambayo sikutumia hata senti nikaenda kumpa Mama
yangu ambaye alikuwa anahitaji lakin moja na nusu ya matibabu”.
Lakini Pia Amber Lulu ameongelea uhusiano wake na Baba yake mzazi ambaye alimkimbia:
"Wanasema
mzazi ni mzazi lakini mimi Baba yangu alinitelekeza kaja kunitafuta
nilivyotoa wimbo wangu wa Watakoma alafu ananiomba hela kusema kweli
aliniumiza kwa sababu hajanitafuta kama miaka kumi halafu anakuja
kunitafuta kwa sababu anataka hela , dah kusema ukweli simpendi baba
yangu hata kidogo na sitaki hata kumuona”
Amber Lulu: Simpendi Baba Yangu Hata KIdogo Na Wala Sitaki Kumuona
Reviewed by RICH VOICE
on
Machi 22, 2018
Rating:
Hakuna maoni