Stormy Daniels: Mwanamke mcheza filamu za utupu anayemtishia Donald Trump
Mcheza filamu za utupu Stormy
Daniels anamshtaki Rais Donald Trump kwa kile kinachoitwa ''hush
agreement'' ambayo ni makubaliano ya kutozungumzia mahusiano yao.
Daniels anadai kuwa yeye na Bwana Trump walikuwa na mahusiano tangu mwaka 2006, lakini alikana shutuma hizo.Kwa nini habari hii ni muhimu?
Stormy Daniels ni nani?
Stormy Daniels alizaliwa Stephanie Clifford, Louisiana mwaka 1979.Alihamia kwenye soko la kucheza filamu za utupu kwanza kama mtumbuizaji, kabla ya hapo mwaka 2004 alikuwa akiongoza na kuandika filamu.
Jina lake la jukwaani,Stormy Daniels, limetokana na jina la binti wa mwanamuziki wa kundi la Mötley Crüe, 'Storm' na jina la kinywaji aina ya Whisky , 'Jack Danniels'.
Unaweza kumtambua kwenye filamu ya 'The 40-Year-Old Virgin' na 'Knocked Up' na video ya muziki wa kundi la Maroon Five 'Wake up call' .
Mwaka 2010 alifikiria kugombea uongozi kwa nafasi ya useneti Louisiana lakini aliahirisha baada ya kusema kuwa ushiriki wake hautiliwi maanani.
Anadai nini?
Mwezi Julai mwaka 2006, Bi Daniels anasema alikutana na Trump kwenye michuano ya hisani ya Golf huko Lake Tahoe, eneo la kujivinjari la kati ya California na Nevada.Katika mahojiano yake na jarida la In Touch Weekly' mwaka 2011 na kuchapishwa mwezi Januari, alisema Trump alimualika chakula cha jioni na kuwa alikwenda kukutana naye kwenye chumba chake cha hoteli.
''Alikuwa amejibwaga kwenye kochi, akitazama televisheni'', alisema kwenye mahojiano hayo, ''alikuwa amevaa nguo za kulalia''.
Bi Daniels anasema walifanya mapenzi kwenye chumba cha hoteli (Mwanasheria wa Trump amesema Trump amekana shutuma hizo)
Kama madai ya mwanadada huyo ni ya kweli, haya yote yangekuwa yametokea miezi minne tu baada ya kuzaliwa kwa mtoto wa Trump mdogo, Barron.
Bi Daniels alisema Trump alimwambia anaweza kumshirikisha kwenye kipindi chake cha Televisheni, The Apprentice.
Amedai kuwa aliangalia sinema ya maisha halisi ya Papa na rais huyo ajaye.
Baada ya hapo anasema waliendelea kuwasiliana kwa miaka kadhaa, Bi Daniels anasema mara ya mwisho kuwasiliana ilikuwa mwaka 2010, wakati alipoahirisha kugombea useneta.
Hata hivyo tetesi kuhusu uhusiano wao zilianza kujionyesha mwezi Novemba 2016 wakati wa uchaguzi wa urais.
Jarida la Wall Street liliripoti siku kadhaa kabla ya kura kuwa bi.Daniels alikuwa kwenye mijadala kwenye kipindi cha asubuhi cha televisheni ya ABC ''Good Morning America'' kueleza yote kuhusu mahusiano yake, kabla ya kuyakata ghafla mazungumzo.
Kwa nini hii ni habari kwa sasa?
Mwezi Januari, Jarida la Wall Street lilichapa makala iliyodai kuwa Wakili wa Trump, Michael Cohen, alimlipa dola za Marekani 130,000 mwanadada huyo mwezi Oktoba mwaka 2016, mwezi mmoja kabla ya uchaguzi.Jarida linasema pesa hizo zilikuwa ni sehemu ya makubaliano ambayo hayakufahamika,ambayo alisema hakuweza kujadili masuala yake mbele ya Umma.
Ripoti nyingi zilitolewa kuhusu hayo lakini shutuma zilikanushwa vikali wakati wakielekea kwenye uchaguzi, maafisa wa Ikulu wameeleza.
Bwana Cohen alikana madai ya kumlipa pesa mwanadada huyo, katika taarifa yake kwenye jarida na kuita shutuma hizo kuwa hazina maana.Na wamekua wakipinga hilo kwa miaka kadhaa.
Lakini mwezi Februari alitangaza kuwa alimlipa Bi.Daniels pesa.
Katika taarifa aliyoitoa kwa New York Times, Bwana Cohen alisema si kampeni za Trump wala Taasisi yake iliyojua chochote kuhusu malipo,ambayo aliyatoa kutoka mfukoni mwake mwenyewe. Alisema hakurejeshewa pesa.
''Malipo kwa Bi Daniels yalikuwa yamefuata sheria'', haikuwa mchango wa kampeni wala si kwa matumizi ya kampeni.
Muda mfupi baada ya makala ya jarida hilo, Bi Daniels alizindua kampeni yake aliyoiita ''Make America Horny Again'' akisafiri kwenda South Carolina kwenye vilabu vya dansi za utupu wakati wa sherehe za maadhimisho ya kuapishwa kwa Donald Trump.
Meneja wa klabu,Jay Levy alisema alihitaji huduma yake, hiyo ilikuwa siku moja baada ya Jarida la the Wall Street kuchapisha makala kuhusu malipo ya dola za kimarekani 130,000.
Kipeperushi kuhusu sherehe hizo kilikuwa kina mzaha kusu mahusiano. Kikieleza ''alimuona moja kwa moja'' ''unaweza kumuona pia''.
Kinachoendelea sasa
Bi Daniels siku ya Jumanne alisema anamshtaki Trump, akidai kuwa hakuweka saini makubaliano yao ya kutoyaweka wazi mahusiano yao.Mwanasheria wake, Michael Avenatti, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuhusu mashtaka yakihusishwa na nyaraka zilizowasilishwa kwenye mahakama ya California.
Siku iliyofuata, ripoti zilisambaa zikisema Rais Trump alishinda kizuizi dhidi ya Bi Daniels.
Amri hiyo ya kizuizi ilimpa marufuku Bi Daniels kutoa taarifa za siri, kuhusu kinachoelezwa kuwa uhusiano wake na Trump.
Stormy Daniels: Mwanamke mcheza filamu za utupu anayemtishia Donald Trump
Reviewed by RICH VOICE
on
Machi 13, 2018
Rating:
Hakuna maoni