Zari: Natafuta Pesa, Sina Muda wa Kutafuta Mpenzi Mpya
Zari
ameibuka na jipya tena huku safari hii akisisitiza kuwa wale wanaume
wakware wote waliopanga foleni kusubiri penzi la Zari hawana nafasi
kwani hana muda wa kuwa na mpenzi kwa sasa.
Zari
alitangaza kumuacha mpenzi wake na Baba watoto wake staa wa Bongo fleva
Diamond Platnumz, mwezi uliopita lakini tangu hapo Kumekuwa na tetesi
nyingi juu ya Zari kupata mwanaume mwingine wa kuchukua nafasi ya
Diamond.
Kupitia
kurasa yake ya SnapChat Zari ameweka wazi kuwa haitaji mpenzi kwa sasa
baada ya marafiki zake kumtumia ujumbe uliosema; “Kama mwanaume wako
akienda kutafuta vimada wenye msambwanda mpya inabidi umkumbushe kuwa
na wewe msambwanda wako mpya ni kwa ajili ya mwanaume mpya”.
Zari amedai kuwa marafiki zake wanamtumia meme hizo kama vijembe kwa EX wake lakini amejibu kuwa hataki mwanaume mpya kwa sasa:
"Marafiki
zangu siwawezi hivi kwanini wamekazana kunionyesha hizi Mambo lakini
hazinifai mimi….. Nahitaji kutafuta pesa mpya na sihitaji mwanaume kwa
muda huu samahani!!!!”.
Zari: Natafuta Pesa, Sina Muda wa Kutafuta Mpenzi Mpya
Reviewed by RICH VOICE
on
Machi 13, 2018
Rating:
Hakuna maoni