Kilichoendelea LEO baada ya IGP, AG na DCI kuitwa Mahakamani Kesi ya Nondo
Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imepanga Aprili 4, 2018 kusikiliza maombi
ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSGN), Abdul Nondo.
Nondo
ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Iringa.
Uamuzi
huo umetolewa leo Machi 21, 2018 na Jaji Rehema Samuje wakati shauri
hilo lilipofikishwa mahakama hapo kwa ajili ya kutajwa.
Hatua
hiyo inatokana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu(THRDC),
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) na Mtandao wa Wanafunzi
Tanzania(TSNP) kuomba mambo matatu ikiwemo Nondo kupewa dhamana.
Jaji Sameja ameutaka upande wa Jamhuri kujibu hoja za utetezi dhidi ya Nondo, Machi 26, 2018.
“Kesi
ya msingi itakuja kusikilizwa April 4 lakini upande wa Jamhuri
mnatakiwa kuja kujibu hoja za upande wa wawasishaji maombi,” alisema
Jaji Sameja.
“Pia upande wa wawasilishaji maombi mnapaswa kuwasilisha maombi ya nyongeza Machi 27, mwaka huu.”
Machi
19, 2018 THRDC, LHRC na TSNP waliwasilisha maombi namba 49, 2018
Mahakama Kuu kutaka itoe amri kwa Jeshi la Polisi kumpeleka mahakamani
Nondo.
Wakili
wa Nondo, Jebra Kambole amedai maombi hayo yalifunguliwa dhidi ya
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Mkuu wa Jeshi la Polisi
(IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo wapeleka maombi wanaiomba
mahakama kutoa amri ya kuletwa mahakamani kwa mwanafunzi Nondo au
kumuachia kwa dhamana kwani ameshikiliwa na polisi kwa muda mrefu bila
sababu za msingi kutolewa.
Kilichoendelea LEO baada ya IGP, AG na DCI kuitwa Mahakamani Kesi ya Nondo
Reviewed by RICH VOICE
on
Machi 21, 2018
Rating:
Hakuna maoni