Viongozi Wakuu CHADEMA Waripoti tena Polisi


Viongozi wanne wa Chadema wamewasili Kituo Kikuu cha Polisi wakiongozwa na Katibu Mkuu Dk  vicenti Mashinji.

Viongozi hao ambao  wamewasili Polisi kwa ajili ya kuitikia wito ni pamoja na manaibu katibu John Mnyika na Salum Mwalimu pamoja na Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti John Heche.

 Wakili wao Fredrick Khiwelo amesema wengine wako njiani akiwamo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Aikaeli Mbowe.

Awali Mbowe  ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai kwa Taifa Leo tarehe 22 Machi 2018, ametoa waraka wa kuitwa Polisi yeye na viongozi wenzake.

Katika waraka huo Mbowe amesema kwamba kuna taarifa pia ya  kumuunganisha  Peter Msigwa,  Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa (Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa) na Mjumbe wa Kamati Kuu katika shauri hili.
Viongozi Wakuu CHADEMA Waripoti tena Polisi Viongozi Wakuu CHADEMA Waripoti tena Polisi Reviewed by RICH VOICE on Machi 22, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...