SINGIDA UNITED YAKANUSHA FIFA KUMFUNGIA STRAIKA WAO, DANIEL LYANGA
Taarifa kuwa mshambuliaji Daniel Lyanga amefungiwa miezi sita na
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kutokana na kusaini mkataba wa
kuitumikia Singida United wakati bado ana mkataba na Fanja SC ya Oman
zimeenea kwa kasi.
Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sangaamekanusha taarifa hiy kwa kusema:
“Ni kweli Daniel Lyanga ni mchezaji wa Singida United na amesajiliwa lakini si kweli kwamba amefungiwa miezi sita (6). Sinida United ilifanya mawasiliano na FIFA pamoja na Fanja kwa hiyo sisi ndiyo wenye taarifa rasmi kuhusu mchezaji huyu ni mali ya nani.
“Wakati tunamsajili Lyanga kipindi cha dirisha dogo mwezi Disemba, 2017, tulimsajili dakika za mwisho baada ya kutoka kwenye michuano ya CECAFA alipokuwa anaitumikia timu ya taifa ya Tanzania bara. Baada ya kukamilisha usajili wake kwa kuwasiliana na timu yake ya zamani (Fanja FC) baada ya kufikia makubaliano na kuwalipa kiasi ya pesa ambacho walikitaka.
“Nyaraka zote za malipo tuliyofanya na Fanja tunazo, release leatter kutoka Fanja tunayo, kwa hiyo unaweza kuona namna taarifa hii isivyo ya kweli kwa sababu huwezi kuwa na release letter ya mchezaji ambaye ana mkataba na timu nyingine.
“Kilichotokea ni kwamba, tulichelewa kupata ITC ya Lyanga na dirisha likawa limefungwa (tanzania) ilikuwa haiwezekani ITC kutumwa kwa wakati huo, kwa hiyo ITC yake bado ipo Fanja na tunategemea kwamba mwezi wa Julai watairuhusu kuja Singida United kwa ajili ya kuitumikia yetu.”
Lyanga hajaonekana kwenye mechi za mashindano rasmi yanayosimamiwa na tff (ligi kuu Tanzania bara na kombe la shirikisho la TFF ‘Azam Sports Federation Cup’) mara ya mwisho kuonekana akicheza mechi za singida united ni kwenye michuano ya Mapinduzi Cup 2018 visiwani Zanzibar.

Reviewed by RICH VOICE
on
Machi 21, 2018
Rating:
Hakuna maoni