Mei Mosi Kitaifa Kufanyika Jijini Arusha....Mgeni Rasmi Anatarajiwa Kuwa Rais Magufuli
Chama
cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na
Ushauri (Tuico), kimeanza maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya
Wafanyakazi Duniani (Mei mosi), yanayotarajiwa kufanyika kitaifa mkoani
Arusha.
Mwenyekiti wa Tuico taifa, Paulo Sangeze, alisema, mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais John Magufuli.
Akizungumza
katika semina ya kuelimisha na kubadilishana uzoefu, iliyowashirikisha
viongozi wa matawi mbalimbali ya Tuico mwishoni mwa wiki, iliyofanyika
jijini hapa, Mwenyekiti wa Tuico taifa, Sangeze, alisema Shirikisho la
Vyama vya Huru vya Wafanyakazi nchini (Tucta), limekiteua chama chao
kuwa mratibu wa shughuli zote za Mei mosi kwa mwaka huu.
Alisema
baada ya kupewa fursa hiyo wanafanya vikao vya maandalizi na tayari
wamepanga maadhimisho hayo kwa mwaka huu, yatafanyika mkoani Arusha
katika Uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.
Katibu
wa Tuico, Boniface Nkakatisi, alisema maandalizi hayo yanaenda na
mialiko ya wageni watakaohudhuria ikiwamo wafanyakazi mbalimbali nchini,
wanachama wa Tuico, mabalozi kutoka nchi mbalimbali duniani.
Mei Mosi Kitaifa Kufanyika Jijini Arusha....Mgeni Rasmi Anatarajiwa Kuwa Rais Magufuli
Reviewed by RICH VOICE
on
Machi 21, 2018
Rating:
Hakuna maoni