Wazee CHADEMA Waomba Kukutana na Rais Magufuli
Baraza
la Wazee wa Chadema limemuomba Rais John Magufuli kukutana na wazee
ili kubadilishana nao mawazo sambamba na kumpa ushauri wa masuala
mbalimbali yanayoendelea nchini.
Akizungumza
leo Jumanne Machi 13, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam, katibu mkuu wa baraza hilo, Roderick Lutembeka amesema
kumekuwa na mambo mengi yanayopigiwa kelele, ni vyema rais akakutana na
wazee ili wamueleza mambo hayo.
“Ni
lazima kama Taifa tuchukue hatua mapema kabla hatujachelewa. Rais
Magufuli akubali kuitikia wito wa kukutana na wazee ambao watakuwa na
ujasiri wa kumshauri ili kuepusha Taifa kuingia kwenye majanga,”
amesema.
Amesema
suala la wazee kukutana na rais, kimekuwa ni kilio cha muda mrefu na
kwamba nchini Kenya viongozi wameweza kukaa meza moja na kumaliza
tofauti zao.
“Lazima
tukae tujue mustakabali wa Taifa hatuwezi kusema hakuna tatizo.
Tunamtaka akutane na wazee, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya
siasa tuzungumze kwa kuwa hii ni nchi yetu wote na si ya chama kimoja,”
amesema.
Amesema mambo yanayopaswa kuzungumziwa ni suala la Katiba Mpya, hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Amesema
pia matukio ya watu kutekwa na kuuawa yameongezeka, “miezi sita
iliyopita tulizungumzia mambo haya lakini naona ndio yanaongezeka.”
“Wazee
tumeumizwa mno kuhusu suala la Abdul Nondo hasa pale Waziri wa Mambo ya
Ndani (Mwigulu Nchemba) alipotoa kauli kuwa kijana huyu alijiteka.
Tulitegemea polisi wafanye uchunguzi, sasa kama waziri mhusika tayari
ameshatoa hukumu tutegemee nini kwa hawa polisi. Tunajenga nini ndani ya
mioyo ya hawa vijana ambao walijitoa kumtetea kijana mwenzao kama si
chuki.”
Wazee CHADEMA Waomba Kukutana na Rais Magufuli
Reviewed by RICH VOICE
on
Machi 13, 2018
Rating:
Hakuna maoni