Waziri Mkuu Atoa Milioni 5 Kwa Mjasiriamali Mlemavu
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemkabidhi Bibi Tecla Hamidu ambaye ni mlemavu wa
miguu sh. milioni tano ili aweze kuongezea katika mtaji wake.
Ametoa
fedha hizo leo (Jumanne, Machi 20, 2018) ikiwa ni katika kutimiza ahadi
yake aliyoitoa Februari 22, 2018 kwenye Mkutano wa Sita wa Wamiliki wa
Viwanda na Watumiaji wa simbomilia (barcodes).
Waziri
Mkuu alitoa ahadi hiyo baada ya Bibi Tecla ambaye ni mjasiriamali
anayejihusisha na ushonaji wa bidhaa mbalimbali zikiwemo nguo kumuomba
amchangie sh. 500,000 ili aweze kuongezea mtaji wake.
Wakati
akimkabidhi fedha hizo, Waziri Mkuu amesema kwamba anatarajia
zitamsaidia katika kuongeza mtaji wake, hivyo atazalisha bidhaa nyingi
zenye ubora unaohitajika katika masoko ya ndani na nje.
Kwa upande wake, Bibi Tecla alimshukuru Waziri Mkuu kwa msaada huo na ameahidi kuzitumia fedha hizo kama ilivyo kusudiwa.
“Nashukuru
kwa msaada huu kwani kuna watu wanakopa sh. laki mbili ili waongeze
mitaji, lakini mimi leo nimepewa milioni tano bure na kiongozi wetu,”
Amesema
licha ya kukabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa masoko anaamini
tatizo hilo litakuwa historia baada ya kuwa na mtaji wa kutosha kwani
atakwenda kuzalisha bidhaa zenye ubora zaidi.
Waziri Mkuu Atoa Milioni 5 Kwa Mjasiriamali Mlemavu
Reviewed by RICH VOICE
on
Machi 20, 2018
Rating:
Hakuna maoni