NACTE yavifungia udahili vyuo 163
Baraza
la Taifa la Elimu na Ufundi (Nacte) limezuia vyuo 163 kudahili
wanafunzi katika kozi mbalimbali ngazi ya astashahada na shahada, baada
ya kukutwa na upungufu ikiwako kutokuwa na walimu wenye sifa.
Akizungumza
leo, Machi 23 na waandishi wa habari, Mkuu wa Ufuatiliaji na Tathmini
wa Nacte, DK Annastella Sigwejo amesema walifanya uhakiki kwa vyuo 459,
kati ya hivyo 296 ndivyo vimekidhi vigezo vya kutoa elimu kwa kiwango
kinachotakiwa.
"Kutokana
na hali hiyo hivyo ndivyo vinaruhusiwa kudahili wanafunzi kwa ajili ya
kozi mbalimbali ngazi ya astashahada na stashahada kwa muhula wa udahili
wa Machi na Aprili mwaka huu.”
Amesema
licha ya kwamba vyuo vilivyosajiliwa viko 580 waliamua kujiridhisha kwa
kuvifanyia uhakiki ambapo walifanikiwa kuhakiki vyuo 459.
Nacte wanawashauri wanafunzi kuhakikisha wanajiridhisha kuwa wanaomba kujiunga kwenye vyuo vilivyokidhi vigezo.
Mkuu wa Kitengo cha Udahili, Twaha Twaha amesema kuwa majina ya vyuo vilivyoruhusiwa kudahili yamewekwa kwenye tovuti ya Nacte.
"Hivyo
Nacte inashauri waombaji wa udahili kujiridhisha kwa kuangalia hiyo
orodha iwapo chuo anachokitaka kinaruhusiwa kudahili,"amesema Twaha.
NACTE yavifungia udahili vyuo 163
Reviewed by RICH VOICE
on
Machi 23, 2018
Rating:
Hakuna maoni