Uingereza yainyooshea kidole Urusi
Waziri
Mkuu wa Uingereza, Theresa May amesema kuwa serikali yake ina amini
kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa Urusi imehusika katika shambulio la
mpelelezi wa zamani wa Urusi, Sergei Skripal na mtoto wake wa kike,
lililotokea kusini mwa Uingereza katika mji wa Salisbury.
Amesema
kuwa inawezekana tukio hilo limefanywa na Urusi ili kuweza kuichafua
Uingereza kwa kushindwa kudhibiti kemikali zake hatari.
“kuna
mambo mawili tu yanaweza kuhusika kwa shambulio lilotokea, inawezekana
serikali ya Urusi ilikusudia kufanya tukio hili hapa Uingereza, ama
imeshindwa kudhibiti silaha hizi hatari za kemikali na hivyo
imesababisha imetumiwa na watu wengine” Amesema May
Aidha,
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson ameiunga mkono
Uingereza kwa kusema kuwa huenda Urusi inahusika moja kwa moja katika
shambulio hilo,
kwa
upande wake msemaji wa ikulu ya Marekani, Sarah Sanders ametoa pole kwa
raia wa Uingereza bila kuunga mkono shutuma ya Uingereza dhidi ya
Urusi.
Hata
hivyo, mbunge kutoka chama tawala nchini Urusi , Vitaly Milonov amesema
kuwa shambulio hilo dhidi ya mpelelezi wa zamani ni mbinu iliyotumika
kuihusisha Urusi na si vinginevyo.
Uingereza yainyooshea kidole Urusi
Reviewed by RICH VOICE
on
Machi 13, 2018
Rating:
Hakuna maoni