Wanachoiga Harmonize na Sarah kutoka kwa Zari na Diamond
Moja ya couple tulivu ambayo haina drama nyingi kwa sasa Bongo ni ile ya Harmonize na mpenzi wake Sarah, wamekuwa pamoja kwa kipindi kirefu sasa tangu pale Harmonize alipoachana na aliyekuwa mpenzi wake Wolper.
Kutokana na utulivu katika mahusiano yao waandishi wa habari za kidaku ni mara chache sana kutupia jicho kujua kile kinachoendelea kati yao ukilinganisha na couple za mastaa wengine ambao waandishi kila uchwao hupata hile na hile kutokana na drama zao.
Sarah ni binti mdogo kutoka nchini Italy ambaye anatajwa kumiliki mkwanja mrefu kwa kiasi chake. Hilo halimzuii kuongozana na muimbaji huyo wa WCB katika show ambazo huenda kuzifanya sehemu mbali mbali.
December 31, 2017 Harmonize alifanya show kubwa sana Mtwara akishirikiana na wasanii kama Shilole, Queen Darleen, Lava Lava Young Killer, Stereo na wengineo. Katika show hiyo Harmonize aliongozana na Sarah mkoani humo kuanzia promotion ya show hadi siku ya tukio lenyewe.
Sarah na Harmonize wakiwa Rwanda
Video Player
00:00
00:57
Kabla ya Diamond na Zari kuachana mara kadhaa walikuwa wakiongozana katika show ambazo alikuwa akifanya muimbaji huyo.
Zari na Diamond wakielekea Naivasha, Kenya kwa ajili ya show
Video Player
00:00
01:00
Baada
ya hapo waliongoza hadi Naivasha nchini Kenya ambapo Diamond pia
alikuwa na show. Hiyo ni mifano tu ya miezi ya hivi karibuni lakini huko
nyuma wamefanya hivyo mara kadhaa.Harmonize na Sarah nao bila shaka kuna vitu viwili vitatu walivipata kutoka kwenye mahusiano ya Diamond na Zari hasa katika upande huo niliyouelezea.
Wanachoiga Harmonize na Sarah kutoka kwa Zari na Diamond
Reviewed by RICH VOICE
on
Machi 23, 2018
Rating:
Hakuna maoni