Necta yafanya mabadiliko mtihani darasa la saba
Mabadiliko
hayo yamefanywa na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) jana na
kutangazwa na Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde.
Ofisa
Habari wa Necta, John Nchimbi amesema mabadiliko hayo aliyatangaza Dk
Msonde katika mkutano mkuu wa tano wa maofisa elimu mkoa na wilaya
unaofanyika Dodoma.
Nchimbi
amesema katika muundo huo mpya kila somo litakuwa na maswali 45, kati
ya hayo, maswali 40 yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi na matano yasiyo ya
kuchagua (yatakuwa ya kujieleza/kuonyesha njia na jibu nk).
Amesema
maswali 40 kila swali litakuwa na alama moja na maswali matano kila
swali litakuwa na alama mbili huku majibu ya maswali 40 yatajibiwa
kwenye OMR FORM na maswali matano yatajibiwa kwenye karatasi maalum
itakayoandaliwa.
Kutokana
na muundo huo mpya, Necta imetoa wito kwa walimu wakuu kuanza kuwapima
wanafunzi kwa kutumia mabadiliko hayo ili kuwajengea uzoefu.
Necta yafanya mabadiliko mtihani darasa la saba
Reviewed by RICH VOICE
on
Machi 21, 2018
Rating:
Hakuna maoni