Rais wa Myanmar Htin Kyaw amejiuzulu
Rais wa Myanmar Htin Kyaw amejiuzulu, kulingana na afisi yake.
Hakuna
sababu ilitolewa lakini kumekuwa na wasiwasi katika miezi ya hivi
karibuni kuhusu afya ya rais huyo mwenye umri wa miaka 71 baada ya
kuonekana amedhoofika katika hafla moja.Htin Kyaw alliapishwa kuwa rais 2016 baada ya uchaguzi uliositisha miongo kadhaa ya uongozi wa kijeshi.
Lakini alikuwa kiongozi asiye na mamlaka huku aliyekuwa kiongozi wa upinzani wa muda mrefu Aung San Suu Kyi akiwa kiongozi mwenye mamlaka.
Taarifa iliochapishwa katika mtandao wa facebook wa rais huyo ilisema kuwa Htin alitaka kupumzika.
Makamu wa rais Myint Swe , jenerali wa zamani atakuwa kaimu rais hadi pale rais mpya atakapochaguliwa katika muda wa siku saba sijazo, taarifa hiyo ilisema.
Bi Suu Kyi, ambaye alifungwa kwa miaka kadhaa chini ya uongozi wa kijeshi wa Junta alipigwa marufuku kuchukua wadhfa huo.
Kipengee cha katiba kilichotengezwa ili kuhakikisha achukui wadhfa huo kinasema kuwa hakuna raia mwenye watoto kutoka nje anaweza kuwa rais.
Alikuwa na watoto wawili na mumewe raia wa Uingereza.
Htin Kyaw alikuwa rafikiye wa utotoni na mshauri wake wa zamnai na wakati mwengine dereva. Alionekana kuwa mtulivu na mtu alimuamini sana.\
CHANZO-BBC SWAHILI
Rais wa Myanmar Htin Kyaw amejiuzulu
Reviewed by RICH VOICE
on
Machi 21, 2018
Rating:
Hakuna maoni