Hatimaye Uingereza yawaruhusu wazazi kumpa mtoto bangi kama tiba
Wazazi wa mtoto mwenye umri wa miaka
6,Alfie Dingley aliye na ugonjwa wa kifafa ambao wamekuwa wakipiga
kampeni ili mtoto wao aruhusiwe kutumia mafuta ya Bangi kupunguza
matatizo ya kifafa, wamesema sasa serikali ya Uingereza imekubali kuwapa
ruhusa ya kutumia bangi hiyo kama tiba.
Wakiongea baada ya
mkutano na Waziri Mkuu Theresa May, Drew Dingley na Hannah Deacon
walisema wamefahamishwa kuwa kijana wao Alfie anaweza kuruhusiwa kutumia
mafuta yatokanayo na mmea Bangi kwa makubaliano maalumu ingawa
matumizi ya Bangi ni kinyume cha sheria nchini Uingereza. Alfie Dingley huanguka kifafa hata mara mia moja na zaidi kila mwezi lakini hali hiyo inaweza kupungua ikiwa atapewa matone matatu ya bangi kwenye ulimi kila siku.
Mama mzazi wa mtoto huyo ameelezea tabu anazozipata, jaziba na hasira ambazo mtoto huyo anamfanyia kutokana na matatizo ya maradhi yake ya kifafa.Ameongeza kuwa watu 380,00 wanaunga ombi hilo na wamewapigia simu familia yao wakidai kuwa wanaridhia wapewe leseni kwaajili ya Alfie Dingley kutumia bangi kwa matibabu.
Hannah Deacon amesema kuwa wamekuwa wakiletewa misokoto mingi ya bangi,watu wakisema wanaelewa tatizo la mtoto.
Hivyo najua wenye mamlaka hawaonji mateso ya maisha ninayo ishi,na wala hawaishi maisha na shida mwanangu,naomba waweke wazi jambo hili.
Muigizaji Sir Patrick Stewart amemwambia mwandishi wa gazeti la Daily Politics Greg Dawson kwamba kwanini anaunga mkono kampeni hiyo.
Hatimaye Uingereza yawaruhusu wazazi kumpa mtoto bangi kama tiba
Reviewed by RICH VOICE
on
Machi 21, 2018
Rating:
Hakuna maoni