Jeshi la Argentina lasitisha zoezi la kutafuta manowari iliyopotea

Matumaini ya kuioata manowari hii iitwayo ARA San kwa sasa yamekufa


Image captionMatumaini ya kuioata manowari hii iitwayo ARA San kwa sasa yamekufa

Jeshi la wana maji la Argentina limesitisha jitihada za kutafuta Monowari iliyopotea kusini mwa bahari ya Atlantiki wiki mbili zilizopita ikiwa na watu 44.
Msemaji wa kikosi cha jeshi la wana maji, Keptein Enrique Balbi amesema kwa sasa shughuli hiyo imeitishwa rasmi.
Kaptain Enrique Balbi, anasema kuwa kikosi cha uokoaji chenye idadi ya watu 4000 kilikwenda kufanya uokoaji mara mbili.

Enrique Balbi amesema hakuna dalili inayoonyesha uwepo wa manowari hiyo
Image captionEnrique Balbi amesema hakuna dalili inayoonyesha uwepo wa manowari hiyo

Balbi anasema kuwa pamoja na jitihada za uokoaji zilizofanyika lakini,hakujawa na mafanikio ya kufanikiwa.
Hata hivyo matumaini ya kuwapa waliokuwa nadani ya nyambizi hiyo wakiwa hai, yalitoweka baada ya kudaiwa kusikika mlipuko mkubwa karibu na eneo ambalo ilikuwa inasadikika kwamba ndipo ilipo manuari hiyo iliyozama.

Manowari hiyo ilikua na watu 44
Image captionManowari hiyo ilikua na watu 44

Nyambizi hiyo ya ARA San Juan ilikumbwa na mkasa huo ilipokuwa ikirejea kutoka katika shughuli zake za kawaida keneo la Ushuaia.
Jeshi la Argentina lasitisha zoezi la kutafuta manowari iliyopotea Jeshi la Argentina lasitisha zoezi la kutafuta manowari iliyopotea Reviewed by RICH VOICE on Desemba 01, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...