Mawaziri wa Mnangagwa waapishwa Zimbabwe

Perence Shiri December 4, 2017 in Harare. / AFP PHOTO / Jekesai NJIKIZANA (Photo credit should read JEKESAI NJIKIZANA/AFP/Getty Images)

Haki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionAlikuwa mkuu wa jeshi la wanahewa Perence Shiri akila kiapo
Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameliapisha baraza lake la kwanza la mawaziri baada ya kuchukua uongozi nchini humo wiki mbili zilizopita.
Rais huyo aliwaondoa mawaziri kadha ambao alikuwa ametangaza kuwateua awali.
Miongoni mwa aliotupa nje ni waziri wa elimu ambaye alikuwa anahudumu chini ya mtangulizi wake Robert Mugabe. Baadhi ya watu walipinga kuteuliwa tena kwake.
Mawaziri wengine waliwatupa nje baada ya kugundua uteuzi wao ulikuwa unakiuka katiba, anasema mwandishi wa BBC mjini Harare Shingai nyoka.
Kwa jumla, mawaziri 21 wamekula kiapo ambao ni mchanganyiko wa wanasiasa ambao wamekuwa uongozini kwa muda mrefu pamoja na wakuu wa kijeshi.
Wakosoaji wanasema uteuzi wa baraza hilo la mawaziri unaonesha jinsi jeshi lilivyodhibiti serikali.
Waziri mpua wa ardhi ambaye alikuwa mkuu wa jeshi la wanahewa Perrance Shiri amepuuzilia mbali madai hayo.
Emmerson MnangagwaHaki miliki ya pichaAFP
"Nilipokuwa jeshini nilikuwa chini ya wizara ya ulinzi ambayo ni sehemu ya serikali. Na nani amesema wanajeshi hawawezi kuwa wanasiasa? Mimi ni raia wa Zimbabwe na nina haki ya kushiriki katika siasa za nchi hii," ameambia BBC.
Mwanajeshi mwingine, Meja Jenerali Sibusiso Moyo ambaye alitangaza kwamba jeshi lingechukua udhibiti wa serikali ameapishwa kuwa waziri mpya wa mambo ya nje na biashara ya kimataifa.
Amesema atahakikisha "uchumi na diplomasia" vinaifaa nchi hiyo.
Rais Emmerson Mngangagwa ameahidi kufanikisha enzi mpya ya ustawi kwa kuimarisha uhusiano kati ya nchi hiyo na nchi za magharibi - ambao ulikuwa umedorora chini ya Bw Mugabe - pamoja na uhusiano wake na wawekezaji kutoka nje ya nchi hiyo.
Bw Mnangagwa alikuwa ametangaza mawaziri ambao wangeteuliwa mapema wiki iliyopita, lakini aliwabadilisha wengine baada ya kugundua kwamba alikuwa amewateua baadhi ambao si wabunge kinyume na maagizo ya katiba.
Baadhi wanasema hiyo ni ishara kwamba rais huyo alikuwa "anawasikiliza wananchi" au kwamba "aliharakisha kufanya jambo hilo muhimu sana."
Mawaziri wa Mnangagwa waapishwa Zimbabwe Mawaziri wa Mnangagwa waapishwa Zimbabwe Reviewed by RICH VOICE on Desemba 04, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...