Mwanafunzi Aliyesambaza Picha za Nyufa Hostel za UDSM Atiwa Mbaroni


Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kumbusho Dawson anashikiliwa na polisi akituhumiwa kusambaza picha kuonyesha nyufa kwenye majengo ya hosteli.

Dawson ambaye ni mbunge wa serikali ya wanafunzi (Daruso) alikamatwa jana Jumatatu Desemba 4,2017 mchana.

Makamu wa Rais wa Daruso, Anastazia Anthony amethibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo jana saa saba mchana.

"Ni kweli Kumbusho alikamatwa jana mchana  na kupelekwa kituo cha polisi cha Chuo Kikuu kwa ajili ya kuhojiwa lakini ilipofika saa tisa alasiri polisi walisema hawana uwezo wa kumuhoji hapa hivyo wakampeleka Oysterbay," amesema Anastazia.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alipotafutwa amesema hana taarifa kuhusu tukio hilo. Alisema anasubiri atakapofikishiwa taarifa atazitoa kwa umma.
Mwanafunzi Aliyesambaza Picha za Nyufa Hostel za UDSM Atiwa Mbaroni Mwanafunzi Aliyesambaza Picha za Nyufa Hostel za UDSM Atiwa Mbaroni Reviewed by RICH VOICE on Desemba 05, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...