Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi apata ajali, avunjika mkono na Kulazwa hospitali ya KCMC

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi baada ya kuvunjika mkono.

Mbatia ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), amevunjika mkono wa kushoto baada ya kuteleza na kuanguka na amelazwa katika wodi za watu mashuhuri (VIP).

Msaidizi wa mbunge huyo, Hamis Hamis alisema jana Jumatano Desemba 20,2017 kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 2:45 usiku wakati akiondoka hotelini kurejea nyumbani.

Hamis alisema Mbatia alikuwa akishuka ngazi katika hoteli ya Uhuru iliyopo eneo la Shanty Town ndipo alipoteleza na kuanguka.
“Bahati nzuri pale kulikuwa na daktari wa KCMC anaitwa Ansbert Sweetbert ndiye alitoa huduma ya kwanza hadi kumpeleka KCMC,” alisema.

Alisema, “Kwa kweli huyo daktari alikuwa msaada mkubwa. Ndiye aliyempeleka KCMC na alikaa naye hadi saa nane usiku. Wauguzi na madaktari KCMC walimpa msaada mkubwa.”
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi apata ajali, avunjika mkono na Kulazwa hospitali ya KCMC Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi apata ajali, avunjika mkono na Kulazwa hospitali ya KCMC Reviewed by RICH VOICE on Desemba 21, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...