Tomas Rosicky astaafu soka ya kulipwa

Mchezaji wa zamani wa Arsenal na taifa la Czech Tomas Rosicky amestaafu soka ya kulipwa

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMchezaji wa zamani wa Arsenal na taifa la Czech Tomas Rosicky amestaafu soka ya kulipwa
Mchezaji wa zamani wa Arsenal na taifa la Czech Tomas Rosicky amestaafu soka ya kulipwa.
Rosicky alijishindia mataji mawili ya kombe la FA na kuichezea Gunners kwa kipindi cha muda wa miaka 10 kutoka Borussia Dortmund 2006.
Raia huyo ambaye alianza soka yake ya kulipwa katika klabu ya Sparta Prague anasema kuwa majeraha yamemlazimu kustaafu.
''Siweze tena kuandaa mwili wangu kwa kiwango cha soka ya kulipwa'', mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 aliambia mtandao wa klabu ya Sparta.
''Mwili wangu ulikuwa ukiniambia kwa muda mrefu kwamba umechoka'', aliongezea Rosicky.
Tomas Rosicky astaafu soka ya kulipwa Tomas Rosicky astaafu soka ya kulipwa Reviewed by RICH VOICE on Desemba 21, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...