Wabunge nchini Uganda kupigia kura mswada wa kurekebisha Katiba


mediaBunge la UgandaReuters
Wabunge nchini Uganda kwa siku ya tatu wanajadili mswada tata wa kuibadilisha Katiba, kuondoa kifungu cha sheria kinachozuia mtu aliye una umri wa miaka 75 kuwania urais nchini humo.
Mswada huo unatarajiwa kupigiwa kura siku ya Jumatano, huku wabunge wa chama tawala NRM wakitarajiwa kuupitisha.
Hata hivyo, wabunge wa upinzani ambao ni wachache, wamesema kwa kauli moja kuwa watapiga kura ya hapana.
Msimamo huu, umeonekana kuwavutia baadhi ya wabunge wa NRM ambao wamesema hawaungi mkono mabadiliko ya katiba baada ya kushauriana
Mbali na marekebisho hayo, baadhi ya wabunge pia wanataka mihula ya uongozi kurejeshwa katika katiba ya nchi hiyo.
Mjadala huu ulioanza siku ya Jumatatu umekumbwa na mvutano kati ya wabunhge wa pande zote mbili lakini pia wasiwasi wa kuwepo kwa maafisa wa usalama katika majengo ya bunge.
Siku ya Jumanne, vikao vya bunge viliahirishwa kwa muda baada ya kuwepo kwa madia ya wanajeshi kuvamia majengo ya bunge.
Wabunge wa upinzani wanasema serikali inatumia wanajeshi kwa lengo la kuleta uoga katika vikao vya bunge ili kupitisha mswada huo kwa nguvu.
Iwapo mswada huo utapitishwa, rais Yoweri Museveni ambaye ameongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 30, atawania tena urais mwaka 2021 akiwa na miaka 76.

Wabunge nchini Uganda kupigia kura mswada wa kurekebisha Katiba Wabunge nchini Uganda kupigia kura mswada wa kurekebisha Katiba Reviewed by RICH VOICE on Desemba 20, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...