Obama aonya kuhusu matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii

Ex-President Obama and Prince Harry at the Invictus games in Canada in September, 29 September 2017

Haki miliki ya pichaPA
Image captionObama alihojiwa na Prince Harry katika BBC Radio 4.
Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama ameonya kuhusu matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii wakati wa mahojiano yasiyo ya kawaida tangu aondoke madarakani mwezi Januari.
Alionya kuwa vitendo kama hivyo vinachanganya uelewa wa watu katika masuala magumu na kusambaza uvumi.
Mrithi wake Donald Trump ni mtumiaji mkubwa wa Twitter lakini Obama hakumtaja jina.
Obama alihojiwa na Prince Harry katika BBC Radio 4.
Prince Harry interviewing President ObamaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionObama alihojiwa na Prince Harry katika BBC Radio 4.
Obama alisema wale walio katika nyadhifa za uongozi wanastahili kuwa waangalifu wakati wanaandika katika mitandao.
Alielezea wasi wasi kuhusu siku za usoni ambapo ukweli utapotoshwa na watu watakuwa wakisema, watakuwa wakisoma na kusikiliza vitu ambavyo vitakuwa vikiridhisha maoni yao.
Bw. Trump amelaumiwa kwa kutumia mtandao wa Twitter kupindukia licha ya yeye kusisitiza kuwa inamruhusu kuwasiliana moja kwa moja na watu wa Marekani.
Obama aonya kuhusu matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii Obama aonya kuhusu matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii Reviewed by RICH VOICE on Desemba 27, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...