Zambia yasitisha ajira ya polisi wa Kichina


Polisi raia wa China waajiriwa Zambia
Haki miliki ya pichaMWEBANTU MEDIA
Image captionPolisi raia wa China waajiriwa Zambia
Maafisa wa polisi nchini Zambia wamefutilia mbali mpango wa kuwaajiri raia wanane wa Kichina kuwa polisi nchini humo yapata saa 24 baada ya kuzindua mpango huo kufuatia pingamizi kutoka kwa raia.
Maafisa hao wapya walikuwa wamepewa jukumu la kupiga doria mjini Lusaka siku ya Jumatatu.
Lakini uamuzi huo ulizua hisia kali kutoka kwa raia hususan kutokana na agizo jipya lililotolewa mapema mwaka huu ambalo linapiga marufuku maafisa wa polisi kuoa wageni kutokana na sababu za kiusalama.
Raia wa Zambia wenye uraia wa mataifa mawili pia hawaruhusiwi kujiunga na kikosi cha polisi.
Dickson Jere, ambaye ni wakili, alisema kuwa uteuzi huo ulikiuka katiba ambayo inasema wazi kuwa, Mzambia yeyote aliye na uraia wa nchi mbili hawezi kujiunga na idara za usalama.
Msemaji wa polisi nchini Zambia Esther Mwata-Katongo, alitetea uteuzi huo wa polisi akisema kuwa kabla ya wao kuteuliwa walichunguzwa na watafanya kazi chini ya usimamizi wa polisi wa kawaida.
Zambia yasitisha ajira ya polisi wa Kichina Zambia yasitisha ajira ya polisi wa Kichina Reviewed by RICH VOICE on Desemba 20, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...