Magolikipa wanaoshikilia rekodi pamoja na David de Gea

David de Gea

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDe Gea alisema tu kwamba: "Ilikuwa mechi nzuri kwangu"
Arsenal walishambulia lango la Manchester United mara 15 Jumamosi, lakini hawakufanikiwa kutikisa wavu isipookuwa mara moja tu - kikwazo chao David de Gea.
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alisema uchezaji wa golikipa huyo wake ulikuwa "bora zaidi duniani".
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger pia alikiri kwamba Mhispania huyo alciheza kwa ustadi mkubwa na kwamba "alikuwa ndiye mchezaji bora wa mechi kwa mbali sana".
Uchezaji wake ulikuwa muhimu sana kwani uliwasaidia kulaza Arsenal 3-1 - na pia ulifikia rekodi Ligi ya Premia.
Hatua yake ya kuzima makombora 14 inamfanya kushikilia rekodi ya kuzuia makombora mengi zaidi mechi moja Ligi Kuu England pwa pamoja na mlindalango wa zamani wa Newcastle Tim Krul na kipa wa zamani wa Sunderland Vito Mannone.
Waliozuia makombora mengi zaidi mechi moja EPL tangu Agosti 2003 (Opta walipoanza kufuatilia data)
TareheTimuMchezajiMpinzaniAliokoa
19 Apr 2014SunderlandVito MannoneChelsea14
2 Des 2017Man UtdDavid de GeaArsenal14
10 Nov 2013NewcastleTim KrulTottenham14
21 Mar 2015West BromBoaz MyhillMan City13
7 Nov 2004FulhamMark CrossleyNewcastle13
2 Jan 2017SunderlandVito MannoneLiverpool13
28 Feb 2016SwanseaLukasz FabianksiTottenham13
8 Apr 2006Man CityDavid JamesTottenham13
Nguzo ya Man City
Kevin de BruyneHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionDe Bruyne aliondoka EPL mara ya kwanza alipoenda Wolfsburg awali kwa mkopo kutoka Chelsea 2012
Kevin de Bruyne, kiungo wa kati wa Manchester City mwenye miaka 26, alisaidia ufungaji wa bao mara ya nane msimu huu ligini.
Alisambaza mpira na kumuwezesha David Silva kufunga mechi ambayo walilaza West Ham 2-1.
Amesaidia ufungaji wa mabao 35 ligini akiwa an City tangu awachezee mechi ya kwanza Septemba 2015.
Hakuna mchezaji mwingine ligi tano kuu za Ulaya (England, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Uhispania) amesaidia ufungaji wa mabao mengi kama yeye. Amemwacha Mesut Ozil wa Arsenal kidogo.
MchezajiAmesaidia kufunga mabao
Kevin de Bruyne (Man City)35
Mesut Ozil (Arsenal)32
Christian Eriksen (Tottenham)30
Luis Suarez (Barcelona)30
Neymar (Barcelona na PSG)29
Lionel Messi (Barcelona)29
Angel di Maria (PSG)27

Mabao ya kujifunga

Lewis Dunk disappointed to score an own goalHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionDunk alijifunga na kuwasaidia Liverpool kulaza klabu yake Brighton 5-1 Jumamosi
Jumamosi, beki wa Brighton Lewis Dunk alijifunga kwa mara ya tatu msimu huu, na kuwasaidia Liverpool kulaza timu yake 5-1.
Ina maana kwamba amejifunga kila mechi tano. Rekodi hata hivyo inashikiliwa na beki wa zamani wa Charlton Richard Rufus ambaye alijifunga mabao matano katika mechi 99.
Richard Rufus of Charlton celebrates scoring a goalHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRufus aliwafungia Charlton mabao sita Ligi ya Premia - hivyo angalau aliwafaa pia kwa mabao
Mabao ya kujifunga Ligi ya Premia (waliojifunga mabao matano na zaidi)
MchezajiMechi alizochezaMabao ya kujifungaMechi kwa kila bao la kujifunga
Richard Rufus99519.8
Michael Duberry161532.2
Martin Skrtel242734.5
Scott Dann194538.8
Neil Ruddock195539
Gareth McAuley199539.8
Richard Dunne4311043.1
Frank Sinclair288648
Wes Brown308651.3
Henning Berg275555
CHANZO :BBC SWAHILI.
Magolikipa wanaoshikilia rekodi pamoja na David de Gea Magolikipa wanaoshikilia rekodi pamoja na David de Gea Reviewed by RICH VOICE on Desemba 04, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...