Serikali yatakiwa kuwachukulia hatua waliovunja haki za binadamu katika uchaguzi

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina sambamba na kuchukulia hatua kali za kisheria, kwa watakao bainika kuhusika na uvunjifu wa haki za binadamu katika uchaguzi mdogo wa madiwani wa marudio wa Novemba 26, 2017 uliofanyika katika kata 43.

Akizungumza na wanahabari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga amesema Kituo hicho kilifuatilis kwa ukaribu uchaguzi huo, na kubainj uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu na taratibu za uchaguzu nchini licha ya kuwa wa huru na haki.

“Kumekuwa na vitendo vya matumizi mabaya ya nguvu ya vyombo vya dola, matukio ya watu kutekwa na wasiojulikana, watu kupigwa, kukamatwa na kujeruhiwa kwa lengo la kuharibu na kuvuruga uchaguzi na kuwatia hofu wapiga kura. Vitendo hivi vimeripotiwa kufanywa na vyombo vya dola, watu wasiojulikana na wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa vyama vya siasa ikiwemo CCM na Chadema,” alisema.

Henga alisema LHRC inatahadharisha kwamba matukio hayo yasipokemewa na jamii in kiashiria kibaya na msingi mbaha utakao athiri chaguzi zijazo ikiwemo wa serikali za mitaa wa mwaka 2019 na Mkuu wa 2020.

“Hii itapelekea kutishwa wapiga kura wasijitokeze kutekeleza haki zao za msingi za kuchagua viongozi wao, kuchochea uhasama miongoni mwa wananchi pamoja na kufifisha imani ya wananchi juu ya vyombo vys usimamizi wa uchaguzu na dola kwa ujumla,” alisema.

Kwa upande wake Mwanasheria wa LHRC, William Benjamin ameitaka serikali kufanya maandalizi ya kimfumo, kikatiba na kisera ili iweze kudhibiti vitendo vitakavyoweza kuharibu uchaguzi.

“Tunashauri mchakato wa katiba urejewe, kuwepo tume huru ya uchaguzi. Vyombo vya dola vijue kazi yake ni kulinda wananchi wanapokuwa kwenye uchaguzi na si kuvuruga uchaguzi,” alisema
Serikali yatakiwa kuwachukulia hatua waliovunja haki za binadamu katika uchaguzi Serikali yatakiwa kuwachukulia hatua waliovunja haki za binadamu katika uchaguzi Reviewed by RICH VOICE on Desemba 01, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...