Kenya yaadhimisha siku kuu ya Jamhuri

Rais Uhuru Kenyatta


Haki miliki ya pichaAFP
Image captionRais Uhuru Kenyatta

Kwa mara ya kwanza sherehe za maadhimisho ya tarehe 12 Disemba, siku kuu ambayo Kenya ilijipatia uhuru, zitafanyika katika uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi Kasarani, Jumanne Disemba 12 mwaka huu wa 2017.
Wakenya wameanza kumiminika katika uwanja huo ulioko katika maeneo ya barabara kuu ya Thika, kilomita 10 kutoka katikati mwa mji mkuu Nairobi, huku usalama ukiimarishwa.
Maadhimisho hayo ya 54 tangu Kenya ilipojipatia Uhuru wake mwaka 1963, yataongozwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Watumbuizaji wa kitamaduniHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWatumbuizaji wa kitamaduni kutoka kwa jamii ya Turkana

Sherehe hizo zitashuhudia, utumbuizaji wa kila aina, ukiwemo nyimbo za kitamaduni na dini, michezo ya kuigiza, mchezo wa kwata, na maonyesho ya ndege za kijeshi pamoja na gwaride maalum ya vikosi vyote vya usalama.
Kwa mjibu wa msemaji wa Serikali Eric Kiraithe, milango ya uwanja huo wa Kasarani itafunguliwa saa moja kamili asubuhi, ili kuwakubalia raia pamoja na watu mashuhuri kuingia tayari kwa sherehe hizo ambazo zitaanza muda mfupi baada ya saa nne mchana.
Sherehe hii ni muhimu kwa Rais Uhuru Kenyatta ambaye aliapishwa majuma mawili yaliyopita kuchjukua hatamu ya miaka mitano ya muhula wake wa pili na wa mwisho uongozini, baada ya kushinda kwenye uchaguzi tata ambao uliosusiwa na upinzani mnamo Oktoba 26.
Kenya yaadhimisha siku kuu ya Jamhuri Kenya yaadhimisha siku kuu ya Jamhuri Reviewed by RICH VOICE on Desemba 12, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...