Wakuu wa jeshi wateuliwa kuwa mawaziri Zimbabwe

Rais Emmerson Mnangagwa amewateua wakuu wa jeshi katika baraza lake jipya la mawaziri


Image captionRais Emmerson Mnangagwa amewateua wakuu wa jeshi katika baraza lake jipya la mawaziri

Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amelitaja baraza lake la mawaziri akimteua afisa mkuu wa jeshi kwa wadhfu mkuu katika serikali yake.
Waziri mpya wa fedha ni Sibusiso Moyo , jenerali aliyetangaza katika runinga ya taifa hilo wiki mbili zilizopita kwamba jeshi limechukua udhibiti.
Mkuu wa jeshi la angani Perence Shiri ataongoza wizara ya fedha na kilimo.
Kiongozi mmoja wa upinzani Tendai Biti amesema kuwa fungate iliokuwa ikisherehekewa Zimbabwe imeisha kabla ya kuanza.
Bwana Mnangagwa aliapishwa wiki moja iliopita kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe ambaye alikuwa mamlakani kwa takriban miaka saba.
Wakuu wa jeshi wateuliwa kuwa mawaziri Zimbabwe Wakuu wa jeshi wateuliwa kuwa mawaziri Zimbabwe Reviewed by RICH VOICE on Desemba 01, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...