Marekani yawawekea vikwazo wataalamu wa makombora Korea Kaskazini

Composite showing North Korean missile developers Ri Pyong-chol and Kim Jong-sik

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKim Jong-sik na Ri Pyong-chol
Marekani imewawekea vikwazo maafisa wawili wa Korea Kaskazini ambao inasema kuwa wamechangia kuundwa makombora ya nchi hiyo.
Wizara ya fedha nchini Marekani iliwataja Kim Jong-sik na Ri Pyong-chol na kusema kwua wote walikuwa viongozi wakuu katika mpango wa makombora ya masafa marefu wa Korea Kaskazini.
Baraza la ulianzi la Umoja wa Mataifa liliiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini siku ya Ijumaa kujibu majaribio yake ya makombora ya masafa marefu.
Korea Kaskazini ilisema kwa hatua hiyo ni kama ya vita.
North Korean leader Kim Jong Un (R) reacts with Ri Pyong Chol (L) in this undated photoHaki miliki ya pichaKCNA/REUTERS
Image captionRi Pyong-chol amepigwa picha akicheka na Kim Jong-un
Vikwazo hivyo vipya vya Marekani vitazuia shughuli zozote za wanaume hao wawili zinazofanywa nchini Marekani, na hata kutwaliwa kwa mali yao yaliyo nchini Marekani.
Wanaume hao wawili wanaonekana mara kwa mara wakiwa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wakiwa maeneo ya kuyafanyia majaribio makombora.
Mwaka huu nchi hiyo imefanya majaribio kadha ya makombora tofauti ambayo nasema kuwa yanaweza kufika nchini Marekani.
Graphic: North Korea's high altitude tests
Image captionMajaribio ya makombora ya Korea Kaskazini


Marekani yawawekea vikwazo wataalamu wa makombora Korea Kaskazini Marekani yawawekea vikwazo wataalamu wa makombora Korea Kaskazini Reviewed by RICH VOICE on Desemba 27, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...