PEP GUARDIOLA AFURAHI MNO MANCHESTER CITY KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA CARABAO

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema anafuraha mno baada ya kikosi chake kutinga kwa ushindi wa matuta 4-3 nusu fainali ya kombe la Carabao Cup dhidi ya Leicester City.

Kipa Claudio Bravo aliyeokoa mikwaju miwili ya penati dhidi ya Wolves katika raundi iliyopita jana pia alipangua penati ya Riyad Mahrez na Jamie Vardy penati yake kugonga mwamba.

Wenyeji ilibidi waende hadi dakika za lala salama ili kukomboa goli moja walilofungwa na Bernardo Silva, na alikuwa Jamie Vardy aliyesawazisha goli kwa mkwaju wa penati.
Mshambuliaji Jamie Vardy akifunga mkwaju wa penati uliofanya mchezo huo uende katika muda wa nyongeza na kuishia kwa matuta
                Kipa wa Manchester City Claudio Bravo akipangua penati ya Riyad Mahrez
PEP GUARDIOLA AFURAHI MNO MANCHESTER CITY KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA CARABAO PEP GUARDIOLA AFURAHI MNO MANCHESTER CITY KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA CARABAO Reviewed by RICH VOICE on Desemba 20, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...