TFF YAMSAFISHA CHIRWA NA KUMRUHUSU KUCHEZA LIGI KUU, MSUVA APEWA ONYO
Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
KAMATI
ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemruhusu kiungo
mshambuliaji wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa kuendelea kucheza Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kumkuta hana hatia kufuatia tuhuma za
kumshambulia refa.
Hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti, Tarimba Abbas jana mjini Dar es Salaam na uamuzi huo unamnufaisha pia kiungo mpya wa Singida United, Deus Kaseke.
Kwa pamoja, wakiwa wachezaji wa Yanga, Chirwa, Kaseke na winga mpya wa Difaa Hassan El- Jadida walidaiwa kumsukuma na kumwangusha refa Ludovic Charles katika mechi namba 236 ya Ligi Kuu iliyokutanisha timu hiyo na wenyeji, Mbao FC walioibuka na ushindi wa 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Hata hivyo, baada ya kikao cha jana, wote Kaseke na Chirwa wamekutwa hawana hatia, huku Msuva pekee akitiwa hatiani na kupewa onyo kali.
Baada ya mchezo huo, Kamati ya Saa 72 ya Bodi ya Ligi ilipitia matukio mbalimbali na kufikia uamuzi wa kuwasimamisha wasubiri suala lao kusikilizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya TFF.
Wachezaji hao walidaiwa kufanya kitendo hicho katika mechi hiyo dhidi ya Mbao FC iliyofanyika Mei 20, 2017 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijni Mwanza. Uamuzi wa Kamati ya Saa 72 ulizingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu.
Lakini refa, Ludovic Charles naye alipewa onyo kali kwa kutoumudu mchezo kwa mujibu wa Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Akizungumza
na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF, Uwanja wa
Karume, Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Peter
Hella amesema kwamba wachezaji wote wapo huru kuendelea na Ligi Kuu
baada ya onyo hilo, lakini wanapaswa kujirekebisha
TFF YAMSAFISHA CHIRWA NA KUMRUHUSU KUCHEZA LIGI KUU, MSUVA APEWA ONYO
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 01, 2017
Rating:
Hakuna maoni