Kwa nini Tundu Lisu Kapelekwa Nairobi Badala ya Muhimbili??......Spika Job Ndugai Katoa Majibu
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai, ametolea
ufafanuzi suala la matibabu ya mbunge wa Singida Mashariki na
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Mh. Tundu Antiphas Lissu aliyepelekwa
Nairobi nchini Kenya baada ya kupigwa risasi.
Akitoa
taarifa hiyo mara baada ya sala ya kuliombea bunge asubuhi ya leo ili
kuanza vikao, Spika Ndugai amesema utaratibu wa matibabu kwa mbunge
yeyote ulikuwa umeshafuatwa lakini familia iliamua yenyewe kumpeleka
Nairobi, na siyo kama walishindwa kumpeleka nchini India.
"Baada
ya bunge kupata taarifa kuhusu tatizo hilo, sisi bunge tulikuwa
tumeshaagiza ndege tayari ilikuwa uwanjani, hapa Dodoma kwa ajili ya
kumpeleka Hospitali ya Muhimbili ambapo ndiyo utaratibu wa kibunge, na
kama kuna rufaa ya nje ya nchi utaratibu wetu ni kwamba serikali yetu
ina mkataba na hospitali ya Apolo kule India, na ndiyo 'channel' ya sisi
wote.
"Lakini
kwa nini mwenzetu alipelekwa Nairobi, ni kwa sababu familia iliomba na
Mh. Mbowe alieleza na mimi nilinukuu kwa niaba yake, walisema siyo kama
wana mashaka na umahiri wa madaktari wetu, lakini wangejisikia faraja
kwa wao wenyewe kuachagua kumpeleka kutibiwa Nairobi", alisema Spika Ndugai.
Spika
Ndugai aliendelea kusema kwamba tukio la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu
ni la kwanza tangu historia ya bunge kuhamia Dodoma kwa miaka mingi, na
kuvitaka vyombo vya dola kushughulikia tatizo hilo, huku akiwaomba
wananchi kuwa watulivu kwani hali yake inatia moyo.
Kwa nini Tundu Lisu Kapelekwa Nairobi Badala ya Muhimbili??......Spika Job Ndugai Katoa Majibu
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 08, 2017
Rating:
Hakuna maoni