Mambo makubwa matano aliyofanya Rais Magufuli Tangu Aingie Madarakani
Na. Paschal Dotto-MAELEZO
Katika
kuelekea ujenzi wa Tanzania ya uchumi wa kati Serikali ya Awamu ya
Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli, Kiongozi anayesifika kwa
uchapakazi, mtu wa watu, mtu wa wanyonge na Mzalendo kwa kusimamia
rasilimali za Taifa ambaye ameonyesha nuru kubwa kwa watanzania.
Katika
hotuba zake mbalimbali amekuwa akisisitiza wananchi kufanya kazi na
kuienzi kauli mbiu yake “HAPAKAZI TU” huku katika utendaji kazi wake
Rais Magufuli ameonesha dira kubwa kwa kuanza na miradi mikubwa ambayo
itaipeleka nchi katika uchumi wa kati na wenye viwanda na huduma nzuri
kwa jamii, watanzania wanatakiwa kumuunga mkono ili aweze kuifanya kazi
yake kwa ufasa kwa kuanzisha, kuendeleza na kumalizia miradi ambayo ipo
mikononi mwake.
Kama
alivyoahidi wakati wa kampeni kwamba Serikali yake itakuwa ya kuchapa
kazi huku akiwa mstari wa mbele katika kuchapa kazi na alipewa jina la
uchapakazi kama Tinga Tinga yani mtu wa kazi, ni miradi mingi ambayo
Serikali yake imefanya na inaendelea kufanya mambo makubwa Kama
yalivyoainishwa na mwandishi wa makala hii.
1. Barabara za Juu (Fly Over).
Aprili
16 ya mwaka 2016 uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara za juu
ulifanyika Jijini Dar es Salaam katika makutano ya barabara ya Tazara
ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli, barabara ambayo itaondoa msongamano wa magari
katika Jiji hilo na kuweza kusaidia kuokoa upotevu wa mapato utokanaona
watu kuchelewa kazini na kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo.
“Faida
kubwa ya barabara hii itatupunguzia fedha zilizokuwa zikipotea, katika
tafiti zilizofanywa mwaka 2013 tulipoteza billion 411.3 katika Jiji la
Dar es Salaam pekee kwa sababu ya msongamano mkubwa”, alisema Rais
Magufuli.
Mradi
huu mkubwa ambao utagharimu fedha za kitanzania shilingi billion 101.6
unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Japan (JAICA), ambapo Shirika
hilo litatoa kiasi cha shilingi billion 93.44 na Tanzania ikitoa billion
8.36,Mradi huu ambao ni wa aina yake Tanzania unatarajia kumalizika
ifikapo oktoba 2018, huku barabara nyingine ya aina hiyo iliyoko
makutano ya Ubungo ikitarajiwa kamilika ifikapo 2020 na kuwezesha wakazi
wa Jiji la Dar es Salaam kufurahia maisha kwani sasa wataondokana na
adha ya usafiri hivyo kuwahi kwenye maeneo yao ya kazi kuchapa kazi na
kuijenga Tanzania ya viwanda.
2. Bomba la Mafuta Ghafi (Hoima-Uganda hadi Chongoleani-Tanzania).
Ilikuwa
ni siku ya pekee kwa wananchi wa chongoleani ambako Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri
Kaguta Mseveni walizindua mradi mkubwa ambao ni wa kipekee duniani.
Ni
bomba ambalo lina urefu wa kilomita 1445 huku Tanzania likichukua
sehemu kubwa yaani kilomita 1115 na kilomita 130 ni kwa upande wa
Uganda, ni mradi ambao utagharimu kiasi cha dola za Kimarekani billion
3.5 na utasimamiwa na kampuni tatu yaani SNOOC,TOTALE zote kutoka nchini
Ufaransa pamoja na TUROL ya Uingereza na unatarijia kukamilika mwaka
2020.
“Ni
mradi wa kipekee duniani kwa kuwa mradi kama huu upo India ambao
unasafirisha mafuta ghafi lakini una kilomita 600 tu, kwa hiyo bomba
hili ni la kwanza duniani”, alisema Rais Magufuli.
Mradi
huu utapita katika Mikoa nane kwa Tanzania bara Wilaya 24 huku Vijiji
184 vikifaidika na mradi huo mkubwa wa kipekee ambao utatoa ajira 10,000
wakati wa ujenzi na 1,000 kwa uendeshaji wake, Wahenga walisema “Kizuri
kula na nduguyo” ndivyo ilivyo kwa Rais Museveni wa Uganda kukubali
kushirikiana katika mradi huu mkubwa kwa kupata ushawishi mkubwa wa
usalama kutoka kwa Rais mchapakazi Dkt.John Pombe Magufuli (Tinga
Tinga).
3. Kufufua Shirika la Ndege (Air Tanzania).
Serikali
ya Awamu ya Tano ilianzisha nia na matumaini katika kukuza na
kuimarisha sekta ya uchukuzi kwa kufufua shirika lake la ndege (ATCL)
ambalo mwaka 2016 lilianza rasmi baada ya Serikali ya Awamu ya Tano
kununua ndege zake mpya ambazo zimekuwa zikisaidia Watanzania hususani
wafanya biashara waendao mikoani mara kwa mara kwa kupunguza gharama
kubwa za usafiri.
“Tumeleta
bombardier Q 400 imepunguza gharama za safari kutoka Dar es Salaam
kwenda Mwanza wanalipa 160,000 hadi 200,000 wakati nauli ilikuwa
imeshafikia hadi 800,000 kwa safari za Dar es Salaam –Mwanza”, alisema
Rais Magufuli.
Mnamo
septemba 2016 serikali ya awamu ya tano ilileta ndege mbili aina ya
Bombadier Q400 ambazo litengenezwa nchini Canada, katika matarajio yake
inatarajia kuwa na ndege 7 ambapo kwa awamu ya kwanza zimekuja mbili ,
lakini pia ndege mbili aina ya Jeti CS 300 zenye uwezo wa kubeba abiria
137-150 zitaletwa nchini 2018 , bila kusahau ndege kubwa aina ya Boen
787-8 Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 262 ambayo nayo italetwa
waka 2018, itasaidia kwa safari za kimataifa kwani itakuwa na uwezo wa
kutoka moja kwa moja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere hadi Marekani ama Ulaya bila kutua kokote.Huu ni mradi ambao
utaleta fursa ya maendeleo hususani katika sekta ya utalii.
4. Sekta ya Utalii.
Sekta
ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe
Magufuli ameendelea kuinua zaidi ni Sekta ya Utalii baada ya ununuzi wa
ndege ambazo zitakuwa kimbilio katika kukuza na kuimarisha Utalii
nchini.
“Huwezi
kuendeleza nchi bila kuwa na Watalii sisi tunazungumza Watalii
hawajaweza kufika hata milioni 2, lakini nchi kama Morocco inapokea
Watalii zaidi ya milioni 12 kwa mwaka kwa hiyo ni vyema kushirikana nao
katika masuala ya Sekta ya Utalii”, alisema Rais Magufuli.
Sekta
ya Utalii ni chachu kwa maendeleo ya Taifa kwani inalipatia pato kubwa
na kuweza kuimarika kiuchumi kupitia fedha za kigeni, lakini kwa
Tanzania kumekuwa na upungufu wa ndege kwa kuliona hilo Serikali ya
Awamu ya Tano imeweza kununua ndege kubwa aina ya Boen 787-8 dreamliner
ambayo itakuwa inatoka moja kwa moja kutoka Ulaya, Amerika na
kwingineko duniani na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
“Tunataka
Watalii wawe wanatoka Marekani wanakuja moja kwa moja Dar es Salaam,
ile ndege inauwezo wa kutoka Marekani, Australia bila kutua popote”,
alisema Rais Magufuli.
Serikali
ya Awamu ya Tano imedhamiria kuendeleza Utalii kwa kuingia makubaliano
na nchi mbalimbali ikiwemo Serikali Morocco kupitia ziara ya Mfalme
Mohammed VI ,ya mwaka 2015 ambapo waliingia makubaliano ya mkataba kwa
Sekta ya Utalii unaolenga kubadilishana Watalii kwani nchi ya Morocco
ina idadi kubwa iliyofikia milioni 12 kwa mwaka 2015 na idadi hiyo
inatarajia kuongezeka mpaka milioni 14 mwaka 2017 kwa hiyo ni vyema kuwa
na ushirikaiano ili kukuza Sekta hii nchini.
5. Mradi mkubwa wa umeme (Kinyerezi I na II).
Juhudi
kubwa za Serikali ya Awamu ya Tano yenye malengo makubwa katika
kuijenga Tanzania kuwa nchi ya viwanda imetambua kuwepo kwa viwanda
kunaambatana na nishati ya uhakika ya umeme kwa hiyo Rais Dkt.John Pombe
Magufuli ameweza kuanzisha mradi mkubwa wa umeme ili kuendana na Sera
yake ya Tanzania ya viwanda.
“Umeme
ni maendeleo, umeme ni kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi kwa Taifa
lolote duniani, bila ya kuwepo kwa umeme wa uhakika ndoto yetu ya
kujenga uchumi wa viwanda haitaweza kutimia”, Rais Magufuli.
Katika
mradi huu wa umeme ulianza na kinyerezi I ambayo itaweza kutoa megawati
150 lakini katika uzinduzi wa ujenzi wa kinyerezi II ambayo itatoa
megawati 240 kwa watanzania, Mradi huu wa kinyerezi II ambao unafadhliwa
na Serikali ya Japan iliyotoa dola za kimarekani milioni 292 ambayo ni
asilimia 85 ya ujenzi huku Tanzania ikitoa dola milioni 120 ambayo ni
sawa na asilimia 15 ya mradi, Uzinduzi huu uliambatana na ongezeko la
megawati kinyerezi I ambapo megawati 180 zitakazogharimu dola milioni 20
jumla ya megawati 330 zitapatikana katika Mradi huo na hii ni faida
kubwa kwa Watanzania wote kwani wataweza kuanzisha viwanda vidovidogo na
hatimaye kukuza uchumi.
“Tunataka
tuwe kama nchi zingine duniani kwa matumizi ya umeme sisi bado tuko
wati 30 kwa kila mtuamiaji wa nishati hii, lakini Kenya wati 40, China
wati 490, Afrika ya Kusini wati 500 na Marekani wati 1,683 kwa kila mtu
kwa hiyo sisi bado tuko nyuma”, Rais Magufuli
Katika mradi huu ambao utajengwa kwa awamu yaani kinyerezi I mpaka VI utasaidia kuondokana na adha ya umeme nchni.
Kwa
uchache hayo ndio baadhi ya mafanikio ambayo JPM ameweza kuyafikia
katika kipindi kifupi alichokaa madarakani, hii ni ishara kuwa hadi
atakapomaliza muhula wake Tanzania itakuwa imepaa kiuchumi na
kimaendeleo katika Nyanja mbalimbali.
Mambo makubwa matano aliyofanya Rais Magufuli Tangu Aingie Madarakani
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 20, 2017
Rating:
Hakuna maoni