Mbunge wa CCM Asimulia Alivyowadhamini CHADEMA Kupata Ndege ya Kumbeba Tundu Lissu Kumpeleka Kenya
Mbunge
wa Mpendae (CCM) Salim Hassan Turky amefunguka na kusema CHADEMA ndiyo
imelipa gharama za ndege iliyombeba Tundu Lissu kutoka Dodoma kwenda
Kenya na kusema yeye aliwadhamini wakati huo kwa kuwa hawakuwa na fedha
taslimu za kulipa
Salim
Hassan Turky ametoa ufafanuzi huo leo baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa
Mbunge huyo ndiye aliyelipia gharama za ndege iliyombeba Tundu Lissu
kutoka Dodoma kwenda Kenya kwa matibabu, taarifa ambayo imetolewa na
Spika wa Bunge jambo ambalo CHADEMA wamelipinga na kusema Spika
anapotosha umma juu ya jambo hilo.
“Tusifanye
tukio la Tundu Lissu kuwa la siasa. Mimi binafsi tukio zima la mbunge
mwenzangu limenisikitisha sana limenisononesha sana. Nikiwa kama
kamishna wa Bunge lakini pia ni binadamu kuna kuzaliwa na kufa,”amesema.
“Kwa hiyo tukio hilo lilipotokea tuliitwa na makamishna wote na Spika wetu wakiwemo Mbowe (Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani) Msigwa na timu yake. Kwanza ndege ilikuwepo pale Airport ambayo ilikuwa imeshaagizwa na Bunge iko stand by kumpeleka moja kwa moja Muhimbili.”
Amesema walichoamua ni kuwa aende moja kwa moja Nairobi nchini Kenya lakini ndege hiyo haikuwa na kibali cha kwenda nchini humo na kwamba ili uweze kwenda nchini humo unalazimika kuwa na marubani wawili.
Hata hivyo, amesema Spika Ndugai alihangaika kupata kibali cha ndege iliyokuwepo uwanjani ili iweze kumpeleka mgonjwa Nairobi.
“Wakati mambo yote tayari rubani wa ndege akasema kuna kitu kinaitwa landing Instrument ambayo ile ndege haina kwa hiyo haitaweza kuruka,” amesema.
Amesema kutokana na majibu hayo waliingiwa na sitofahamu watafanya nini lakini yeye aliingia katika uzoefu wake aliopewa na Mungu kwa kutafuta ndege kwa ndugu zake ambao wanafanya nao biashara sana.
“Nikawaambia ndege ipo wakatoa nauli zao za ghali ghali kwa sababu tunajuana wakakubali kutusaidia kwa dola 9,200 pamoja na ambulance (gari la wagonjwa) mimi ndio niliyoita kwa kubaliana na Mbowe na Msigwa kwamba Turky haya mambo yasimamie baadaye…na ndicho kilichofanyika,” amesema.

Aidha
Turky aliendelea kueleza kuwa walipofika nchini Kenya siku ya pili
walipaswa kuwa ametoa fedha hizo lakini haikuwa hivyo mpaka leo Septemba
14, 2017 majira ya saa sita mchana alipowasiliana na wahusika aliambiwa
kuwa CHADEMA walikuwa wameshalipa hizo fedha.
Mbali
na hilo Turky amesema kuwa kauli ambayo Spika wa Bunge Job Ndugai
ameisema leo bungeni haikuwa na tatizo kwani alikuwa amesema yeye ndiye
amelipa hiyo fedha lakini CHADEMA wangekuja kuirudisha kwake, jambo
ambalo anadai kama leo wasingeweza kulipa CHADEMA basi angelipa yeye
fedha hizo kwa watu hao halafu yeye angekuja kumalizana na CHADEMA.
Pia
katika kauli ambayo ametoa Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa amesema
kuwa fedha hizo za ndege iliyombeba Tundu Lissu kutoka Dodoma kwenda
Nairobi nchini Kenya imelipwa na Watanzania ambao walikuwa wanachangia
fedha za matibabu kwa Lissu pamoja na CHADEMA wenyewe na si mbunge wa
CCM.
Mbunge wa CCM Asimulia Alivyowadhamini CHADEMA Kupata Ndege ya Kumbeba Tundu Lissu Kumpeleka Kenya
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 14, 2017
Rating:
Hakuna maoni