Hussein Bashe: Amani Imepoteza, Hakuna Aliye na Uhakika na Maisha Yake
Mbunge
wa Nzega Mjini Hussein Bashe amefunguka na kuomba muongozo wa Spika
kuhusu hali ya usalama wa nchi, kwa kuwa matukio ambayo yanaendelea
kutokea ya kihalifu hayana hitimisho yake.
Bashe
amesema hayo wakati akiomba muongozo ndani ya bunge kwa kumtaka Spika
wa bunge Job Ndugai kukubali ombi la kamati ya usalama ya bunge likutane
na vyombo vya usalama ili yaweze kupatikana majibu ya matukio
yanayoendelea kutokea.
"Mhe.
Spika katika taifa letu katika kipindi cha muda mrefu kumekuwa
yakitokea matukio mbalimbali ambayo sisi kama wawakilishi wa wananchi
tuna wajibu wa kupata taarifa sahihi juu ya muendelezo wa matukio hayo
ambayo hayana hitimisho", amesema Bashe.
Pamoja
na hayo, Bashe aliendelea kwa kusema "sisi tunawawakilisha Watanzania
milioni 50 lakini matukio haya yanayotokea yanaharibu heshima ya taifa
letu ningekuomba kama utaridhia na wabunge wataniunga mkono, uitake
kamati yako ya ulinzi na usalama ya bunge tukufu ikutane na vyombo vya
ulinzi na usalama ili tuweze kupata taarifa kamili juu ya mambo haya
yanayoendelea katika taifa letu, ili Watanzania na sisi wabunge tuwe na
uhakika kwa sababu hali inavyoendelea hakuna mtu mwenye uhakika na
maisha yake ya kesho. Dhamana tuliyopewa sisi dhamana ya kusimamia mali,
usalama pamoja na raia wa nchi hii", amesisitiza Bashe.
Kwa
upande wake Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai alikubali hoja iliyotolewa
na mbunge Bashe na kutoa amri kwa kamati ya ulinzi na usalama ya bunge
iende kukutana ili wapange ni jinsi gani ya kulishughulikia jambo hilo
na watakapokuwa tayari kabla bunge kuhairishwa siku ya Ijumaa wiki ijayo
warudishe majibu kwa bunge juu ya walichoamua.
Hussein Bashe: Amani Imepoteza, Hakuna Aliye na Uhakika na Maisha Yake
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 10, 2017
Rating:
Hakuna maoni